Pata taarifa kuu

Kenya: Kongamano la Connected Afrika linaendelea jijini Nairobi

Wadau kwenye sekta ya teknolojia na mawasiliano, wanaendelea kukutana jijini Nairobi kwenye kongamano la Connected Africa, wanakojadiliana namna ya kuendelea kutumia maendeleo ya teknolojia kuimarisha biashara na uchumi barani Afrika. Victor Moturi amehudhuria kongamano hilo na kuandaa ripoti hii.

Wadau kwenye sekta ya teknolojia na mawasiliano, wanaendelea kukutana jijini Nairobi kwenye kongamano la Connected Afrika.
Wadau kwenye sekta ya teknolojia na mawasiliano, wanaendelea kukutana jijini Nairobi kwenye kongamano la Connected Afrika. © Connected Africa Summit
Matangazo ya kibiashara

Kwenye mkutano huu wa Connected Afrika unaofanyika jijini Nairobi  nchini Kenya ambao  uliowaleta pamoja viongozi wa mataifa na washikadau vile vile wavumbuzi wa teknolojia,,,uvumbuzi umeonakana kupigiwa upato huku mataifa mengi Afrika sasa yakionekana utengenezaji wa  bidhaa za teknoljia badala ya kuagiza kutoka ughaibuni.

Rono Nicholas ni miongoni mwa wanaohudhuria kongamano hili jijini Nairobi.

“Sisi tunaunda cable inaitwa fibre optic inayopitisha mtandao kwa nyumba na ofisi na naona sasa hivi nchini Kenya hali imeanza kuwa tofauti kiasi maana hawapo awali hapakuwa na kiwanda.” alisema Colasha Nicholas kutoka kampuni ya Nia Fibre.

00:15

Rono Nicholas ni Mkuu wa kampuni ya Nia Fibre

Ripoti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (International Finance Corporation) inatabiri kuwa uchumi wa mtandao barani Afrika unaweza kufikia dola bilioni 180 ifikapo mwaka 2025, ikichangia asilimia 5.2 ya pato la Taifa la bara hilo. Kufikia mwaka 2050, iwapo uvumbuzi wa mitandao utazingatiwa pakubwa.

“Zinawasaidia sana vijana kupata kazi ya mitandaoni na zile za akili mnameba na nyenginezo.” alisisitiza Colasha Nicholas kutoka kampuni ya Nia Fibre. 

00:08

Rono Nicholas kuhusu connected Afrika

Hata hivyo uimarishaji wa intaneti katika maeneo ya mashinani barani Afrika bado ungali nchini mno ukilinganisha na mijini,huku washakadau wakiombwa kuangazia maeneo hayo kikamilifu.

George Njuguna ni kutoka kampuni ya maswasailiano ya safaricom nchini Kenya.

“Tunaleta mambo mapya kwa wanachi wetu ambapo wanaweza kufanya biashara zao na kuzungumza na kufanya mawasiliano katika nchi za kigeni.” Alisema George Njuguna.

00:09

George Njuguna ni kutoka kampuni ya mawasiiano ya safaricom

Mkutano huu wa connected Afrika,unalenga kuboresha miundo mbinu za intanenti barani Afrika,kupiga jeki kupitia chumi zinazotokana na mitandao,kuimarisha uvumbuzi huku kauli mbiu ikiwa Kuinua mustakabali wa Afrika kupitia mtandao na kuinua ukuaji zaidi  kupitia mawasiliano.

RFI

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.