Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

DRC: Watu zaidi ya 5 wauawa katika shambulio la mabomu Kimachine

Watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa kundi la M23, kutoka ngome zao za juu katika eneo la Masisi, wamerusha mabomu katika kambi ya watu waliotoroka makaazi yao huko Kimachine, kwenye barabara ya Goma-Sake.

[Picha ya kielelezo] Wakongo wakiwa wamebeba mali zao wakitoroka vijiji vyao karibu na Sake, katika eneo la Masisi, kufuatia mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC), kuelekea Goma, mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
[Picha ya kielelezo] Wakongo wakiwa wamebeba mali zao wakitoroka vijiji vyao karibu na Sake, katika eneo la Masisi, kufuatia mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC), kuelekea Goma, mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. REUTERS - ARLETTE BASHIZI
Matangazo ya kibiashara
01:40

KIMASHINE

Mlipuko huo,umesababisha vifo vya watu zaidi ya 5 na takriban ishirini wamejeruhiwa, ambao wamepelekwa hadi katika hospitali ya CEBCA Ndosho jijini Goma, kulingana na ripoti ya muda iliyotolewa na vyanzo kwenye eneo hilo.

Hayo yanajiri wakati waasi wa M23, wakiungwa mkono na jeshi la Rwanda kulingana na vyanzo mbalimbali vikinukuliwa na Radio OKAPI, wamedhibiti mji wa madini wa Rubaya, eneo la Masisi katika mkoa wa Kivu Kaskazini, tangu Jumanne Aprili 30.

Mkuu wa idara ya madini katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Yvette Mwanza, anathibitisha kuwa kutokana na uvamizi wa mgodi huu, mapato makubwa hayataingia katika hazina ya serikali.

Kulingana afisa huyo, mgodi wa Rubaya ndio kitovu cha uchumi wa sekta ya madini huko Kivu Kaskazini katika suala la mapato ya mkoa:

"Uzalishaji wa Coltan katika Rubaya pekee unawakilisha 50% ya uzalishaji wa kitaifa."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.