Pata taarifa kuu

Msumbiji: Wanajihadi wa kiislamu waliwatumia watoto kutekeleza mashambulio

Wanajihadi wa kiislamu wanaoendesha shughuli zao katika jimbo la kaskazini la Cabo Delgado nchini Msumbiji, liliwatumia wavulana wenye umri wa miaka 13 kutekeleza mashambulio kwenye mji huo wiki iliyopita, imesema ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch.

Makundi yenye silaha kwa muda sasa yamekuwa yakitekeleza mashambulio katika eneo la kaskazini mwa Msumbiji.
Makundi yenye silaha kwa muda sasa yamekuwa yakitekeleza mashambulio katika eneo la kaskazini mwa Msumbiji. © RFI/Lígia Anjos
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Al-Shabab, ambalo ni mfuasi wa Islamic State, hapo awali lilishutumiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kuwateka nyara watoto na kuwatumia kama wanajeshi katika uasi wake kwenye eneo hilo.

Kuongezeka kwa mashambulio ya wanajihadi tangu mwezi Machi mwaka huu, kwa uchache watoto 70 wameripotiwa kupotea, kulingana na mamlaka za serikali ya mitaa na mashirika ya misaada.

Walioshuhudia wameliambia shirika hilo kuwa makumi ya watoto walitumiwa katika mashambulio hayo na walionekana wakiwa wamebeba bunduki aina ya AK 47 na mikanda ya risasi.

Mashirika ya misaada yanasema mzozo huu uliwalazimisha zaidi ya watu milioni moja kuyakimbia makazi yao tangu Oktoba 2017 na maelfu wameuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.