Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Wanajeshi wanane wahukumiwa kifo kwa 'kumkimbia adui' nchini DRC

Wanajeshi wanane wa DRC, wakiwemo maafisa watano, wamehukumiwa kifo kwa "uoga" na "kukimbia adui" siku ya Ijumaa na mahakama ya kijeshi huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako waasi wa M23 wanaendelea kusonga mbele na kudhibiti baada ya maeneo.

Kulingana na utetezi wao, wanajeshi hawa "hawakuwahi kumkimbia adui, wala kutelekeza ngome yao". Lakini mahakama imeamua kwamba makosa dhidi ya wanane kati yao yamezingatiwa" kulingana na shahidi na vielelezo vilivyotolewa".
Kulingana na utetezi wao, wanajeshi hawa "hawakuwahi kumkimbia adui, wala kutelekeza ngome yao". Lakini mahakama imeamua kwamba makosa dhidi ya wanane kati yao yamezingatiwa" kulingana na shahidi na vielelezo vilivyotolewa". RFI/Lea Westerhoff
Matangazo ya kibiashara

Upande wa mashtaka ulikuwa umeomba adhabu ya kifo dhidi ya askari 11 walioshtakiwa katika kesi hiyo, lakini mahakama iliwaachilia huru askari watatu wa vyeo vya chini, ikizingatiwa kwamba mashitaka dhidi yao "hayajathibitishwa".

Wote walikuwa mstari wa mbele katika mapigano dhidi ya waasi wa M23 ("March 23 Movement") ambao, kwa kuungwa mkono na vikosi vya jeshi la nchi jirani ya Rwanda, wameteka maeneo makubwa ya mkoa wa Kivu Kaskazini kwa kipindi cha miaka miwili.

Kulingana na utetezi wao, wanajeshi hawa "hawakuwahi kumkimbia adui, wala kutelekeza ngome yao". Lakini mahakama imeamua kwamba makosa dhidi ya wanane kati yao yamezingatiwa" ulingana na shahidi na vielelezo vilivyotolewa".

Uamuzi huu unakuja wakati serikali ya DRC ilitangaza katikati ya mwezi Machi uamuzi wake wa kuondoa usitishaji wa utekelezaji wa hukumu ya kifo ambayo imekuwa ikitekelezwa tangu mwaka 2003 nchini humo.

Ilieleza kuwa hatua hii ililenga askari wanaotuhumiwa kwa uhaini na wahalifu wa "ujambazi wa mjini unaosababisha kifo cha mtu". Kushindwa kwa jeshi la Kongo na wanamgambo wake wasaidizi mbele ya M23 kumezua tuhuma miongoni mwa viongozi kwa kutoroka kwa vikosi vya usalama.

Tangu kutokea kwa uasi huu, wanajeshi wengi, wakiwemo maafisa wakuu wa FARDC (Vikosi vya Wanajeshi wa DRC), lakini pia wabunge, maseneta na watu binafsi kutoka katika ulimwengu wa kiuchumi Mashariki mwa DRC, wamekamatwa na kushutumiwa kwa "kushirikiana" na adui”.

Akiwa ziarani mjini Kinshasa katikati ya mwezi wa Aprili, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Volker Türk, alisema "anatiwa wasiwasi" na uamuzi huu wa mamlaka ya Kinshasa, akikumbusha kwamba Umoja wa Mataifa ulitaka "kukomeshwa kwa hukumu ya kifo duniani kote.

Akihojiwa na televisheni ya Ujerumani Deutsche Welle mwishoni mwa mwezi wa Aprili, Rais wa DRC Félix Tshisekedi alitangaza kwamba DRC imechukua uamuzi huu "kuwakatisha tamaa" washirika wa Rwanda. "Ikiwa wataendelea, adhabu ya kifo itatumika kwao," alihakikisha.

Kwa zaidi ya miaka 20, hukumu za kifo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara nchini DRC, hasa katika kesi zinazohusisha wanajeshi au wapiganaji wa makundi yenye silaha, lakini zilibadilishwa kwa utaratibu na kuwa kifungo cha maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.