Pata taarifa kuu

Macron aitaka Rwanda 'kusitisha msaada wake' kwa M23 na 'kuondoa vikosi vyake' DRC

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameitaka Rwanda mnamo Aprili 30, 2024 "kusitisha msaada wake" kwa waasi wa DRC wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na "kuondoa vikosi vyake" nchini humo. Kwa upande wake, Rais wa DRC, Félix Tshisekedi, katika ziara yake  rasmi huko Paris mnamo Aprili 29 na 30, 2024, alitangaza kwamba "jeshi la Rwanda linapaswa kuondoka kwenye ardhi ya Kongo" ili "iwezekane kujadili" na Kigali. 

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Félix Tshisekedi na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mnamo Aprili 30, 2024 huko Paris.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Félix Tshisekedi na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mnamo Aprili 30, 2024 huko Paris. © Élysée
Matangazo ya kibiashara

"Rwanda, na nilisisitiza hili kwa Rais Paul Kagame katika mazungumzo ya hivi majuzi, lazima ikomeshe uungaji mkono wake kwa M23 na kuondoa majeshi yake katika eneo la Kongo. » Kwa hivyo rais wa Ufaransa alioanisha msimamo wake na washirika kadhaa wa Magharibi ambao tayari walikuwa wametoa matamko kama hayo.

DRC na Ufaransa zilitaka kusahau mjadala mkali wakati wa ziara ya rais wa Ufaransa mjini Kinshasa mwaka mmoja uliopita, na ilifanikiwa. Jumanne hii, Aprili 30, 2024, wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, baada ya chakula cha mchana, marais hao wawili walionyesha uelewa wao. Ni lazima kusema kwamba wakati huo huo, msimamo wa Ufaransa umebadilika juu ya suala la Kivu Kaskazini. Emmanuel Macron ametoa wito wa "kusitishwa kwa mapigano" katika eneo hili lililokumbwa na ghasia kutoka kwa makundi kadhaa yenye silaha, ikiwa ni pamoja na waasi wa kundi la Machi 23 (M23) linaloungwa mkono na Kigali.

"M23 ni ganda tupu ambalo Rwanda hujivika"

Félix Tshisekedi, katika ziara rasmi ya Aprili 29 na 30, alithibitisha kwamba nchi yake inaweza "kutegemea Ufaransa, ambayo itakuwa upande wetu kupata" amani mashariki mwa DRC. "Kilichonivutia zaidi ni kujitolea zaidi kwa Ufaransa kwa kile tunachoteseka kama vita vya dhuluma vilivyowekwa kwetu na Rwanda, ambayo inaunga mkono M23," anasisitiza Rais Tshisekedi. Nadhani, kwa majadiliano tuliyokuwa nayo leo, kuna mwanga wa matumaini juu ya upeo wa macho. "

Anaongeza kuwa "M23 ni ganda tupu ambalo Rwanda inavaa" na kwamba "jeshi la Rwanda lazima liwe limeondoka kwenye ardhi ya Kongo" ili "kuweza kujadili, lakini kujadiliana kukubaliana kwamba Rwanda haina cha kufanya zaidi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa upande wake, Ufaransa inaangazia uhusiano wake mzuri na nchi hizo mbili zinazozozana kujaribu kutafuta suluhu la mgogoro huu. Mkuu wa nchi wa Ufaransa amesisitiza kuwa "ni muhimu, wakati huo huo, kupigana dhidi ya matamshi ya chuki na hatua ya waasi wa zamani wa FDLR", kundi la waasi wa Kihutu ambalo awali liliundwa na watu waliohusika katika mauaji ya halaiki ya nchini Rwanda. Rais wa Ufaransa alimshukuru mwenzake wa Kongo kwa kujitolea kupigana na kundi hili lenye silaha. Ahadi ya shukrani ambayo Emmanuel Macron anatangaza "kuwa na nguvu za kutosha kuishawishi Rwanda kuondoa majeshi yao ambayo hayana la kufanya katika ardhi ya Kongo".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.