Pata taarifa kuu

Washington inaamini Angola inaweza kufanikisha upatanisho kati ya DRC na Rwanda

Marekani imeeleza matumaini ya Angola kufanikisha upatanisho kati ya rais wa Rwanda Paul Kagame na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ili kumaliza mvutano kati ya nchi hizo.

Uhusiano kati ya DRC na Rwanda umeonekana kuzorota zaidi baada ya shambulio kwenye kambi ya wakimbizi wa Mugunga.
Uhusiano kati ya DRC na Rwanda umeonekana kuzorota zaidi baada ya shambulio kwenye kambi ya wakimbizi wa Mugunga. AFP - JORGE NSIMBA
Matangazo ya kibiashara

Mwanadiplomasia na naibu waziri wa maswala ya Afrika ,nchini Marekani ,Molly Phee ,akizungumza katika kikao cha bunge la Congress ,amesema rais wa Angola Joao Lourenco yuko mbioni kuwasisitizia viongozi hao ,kuheshimu mwongozo wa amani uliokubaliwa na Marekani pamoja na viongozi wa ukanda.

Aidha, Phee amesema Marekani inaupa kipau mbele mkakati wa kuzuia mauaji zaidi katika mashariki mwa DRC baada ya shambulio la mabomu Mei tarehe tatu katika kambi ya wakimbizi ya Mugunga lilosababisha maafa na majeruhi.

Rais wa Angola Joao Lourenco na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi wamekuwa wakitafuta suluhu ya kinachoendelea mashariki ya DRC.
Rais wa Angola Joao Lourenco na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi wamekuwa wakitafuta suluhu ya kinachoendelea mashariki ya DRC. © RDC

Angola ambayo ni mshirika mkubwa wa Marekani, imekuwa ikiongoza juhudi za upatanisho na kurejesha amani nchini DRC na Machi mwaka huu, ilisema rais Kagame na Tshisekedi walikuwa wameafikiana kufanya mazungumzo ya ana kwa ana.

Hata hivyo Marekani imeeleza matumaini ya Angola kufanikisha upatanisho kati ya rais wa Rwanda Paul Kagame na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ili kumaliza mvutano kati ya nchi hizo.

Soma piaDRC : Mazishi ya wakimbizi waliouwa katika kambi ya Mugunga yamefanyika

Marekani pamoja na DRC zinaamini Rwanda ilihusika au kushirikiana na waasi wa M23 katika shambulio hilo lakini Rwanda inakanusha madai hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.