Pata taarifa kuu

DRC: Uchunguzi wafunguliwa baada ya wabunge kutoka chama cha rais kupewa magari

Nchini DRC, mashirika ya kiraia yanashutumu utoaji wa magari kwa wabunge wa mkoa wa Kinshasa. haya ni magari aina ya jeep zilizotolewa na chama cha Rais Félix Tshisekedi kwa wabunge waliochaguliwa wa chama chake, siku moja kabla ya uchaguzi wa maseneta, magavana na manaibu gavana. utoaji wa magari haya unaoelezewa kama rushwa na mashirika ya kiraia. Idara za usalama zimefungua uchunguzi.

Maafisa wa polisi katikati mwa jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Februari 12, 2024.
Maafisa wa polisi katikati mwa jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Februari 12, 2024. REUTERS - ANGE KASONGO ADIHE
Matangazo ya kibiashara

Idara ya ujasusi nchini DRC imekamata takriban magari kumi na kuwakamata maafisa kadhaa wa usalama, akiwemo afisa wa polisi. Alikuwa na jukumu la kulinda magari kadhaa yaliyohifadhiwa katika jengo la Gombe, takriban mita mia moja kutoka makao makuu ya kitengo cha polisi ya uchunguzi.

Wakati wa kukamatwa kwa magari hayo, afisa mkuu wa kisiasa anaamini, idara ya ujasusi haikufahamishwa kuwa magari haya yalitoka kwa chama cha rais. Ilikuwa ni Jumanne pekee ambapo mkuu wa chama cha rais, Augustin Kabuya, alieleza haya. Kwake, ni bonasi ya motisha "kutoa motisha kwa viongozi waliochaguliwa, mchango kwa ajili ya faraja, baadhi ya viongozi waliochaguliwa husafiri kwa teksi au pikipiki".

Siku ya Alhamisi, ACAJ, shirika la kiraia, liliona kuwa haikubaliki kwamba katibu mkuu wa UDPS anaweza kuhalalisha kile linachoeleza kama "ufisadi wa wabunge wa mkoa wa Kinshasa siku moja kabla ya uchaguzi". ACAJ inakumbuka kwamba Mkuu wa Nchi mwenyewe alikemea kutowajibika kwa vyombo vya sheria na kuvitaka kukabiliana na vitendo vya rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.