Pata taarifa kuu

MONUSCO yamaliza operesheni zake katika mkoa wa Kivu Kusini

Wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO), wamemaliza rasmi operesheni zao katika mkoa wa  Kivu Kusini, mashariki mwa nchi, baada ya miaka 20.

Wanajesi wa MONUSCO wakishika doria wakati wa ujumbe wa usalama huko Kitshanga, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 11 Desemba 2022.
Wanajesi wa MONUSCO wakishika doria wakati wa ujumbe wa usalama huko Kitshanga, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 11 Desemba 2022. © AFP - Guerchom Ndebo
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mipango yao, MONUSCO ilikuwa ifunge shughuli zake katika mkoa huo kuanzia tarehe 1 mwezi Mei.

Baada ya kuondoka Kivu Kusini, walinda amani amani hao wataendelea na operehseni zao katika mkoa wa  Kivu Kaskazini na Ituri, wakati huu wakiwa na mpango wa kuondoka kabisa nchini humo kufikia mwisho wa mwaka huu.

Hivi karibuni msemaji wa MONUSCO Luteni Kanali Kedagni Menhsah alisema MONUSCO kwa upande wake imejizatiti kutekeleza mamlaka mpya iliyopatiwa kuhusu awamu za kuondoka DRC, huku ikiruhusu jeshi la kitaifa la ulinzi na usalama kurejea kwenye majukumu yake kwa kujitegemea.

Kituo cha MONUSCO cha Kamanyola, huko Kivu Kusini ambacho kilikuwa kinatumiwa na walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa kutoka Pakistani kilifungwa tarehe 28 mwezi Februari mwaka huu na majengo yake kukabidhiwa ka Polisi wa kitaifa nchini humo, CNP.

Walinda amani wa UN wamekuwa wakituhumiwa kwa kushindwa kuwajibikia wajibu wao.
Walinda amani wa UN wamekuwa wakituhumiwa kwa kushindwa kuwajibikia wajibu wao. © Glody Murhabazi / AFP
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.