Pata taarifa kuu
UHURU-VYOMBO VYA HABARI

Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani: Wanahabari wakumbwa na changamoto nyingi DRC

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari leo Ijumaa April 3, wanahabari nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza kazi yao, hasa wakati huu nchi hii ikikabiliwa na mdororo wa usalama mashariki mwa nchi.

Vitisho vya makundi ya watu wasiojulikana dhidi ya waandishi wa habari,imekuwa pia  ni changamoto kubwa zinazo wakabili wanahabari hao wakimbizi anaongeza.
Vitisho vya makundi ya watu wasiojulikana dhidi ya waandishi wa habari,imekuwa pia ni changamoto kubwa zinazo wakabili wanahabari hao wakimbizi anaongeza. Photo MONUSCO/Anne Herrmann
Matangazo ya kibiashara

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, utovu wa usalama Mashariki mwa nchi hiyo umesababisha wanahabari zaidi ya 100 kuacha kazi na kukimbia kwa kuhofia usalama wao.

Kama vile wengine wanavyohangaika katika mji wa Goma, Darleine Rushago, mwandishi wa habari aliyekimbia mafichoni baada ya waasi wa M23 kuchukuwa udhibiti wa mji wa Rutshuru  anaeleza wanakabiliwa na changamoto nyingi.

"Tangu kutoroka mji wetu wa Rutshuru hali ya maisha sio nzuri kabisa mwenyewe unafahamu kwamba kila mtu hujihisi vizuri akiwa nyumbani kwao. Tumeshindia jinsi yakutafuta maisha sababu hata msaada hatupati ,kulikuwa na wafadhili waliotutolea msaada wakati tuliwasili Goma lakini kwa sasa hakuna ".

Vitisho vya makundi ya watu wasiojulikana dhidi ya waandishi wa habari,imekuwa pia  ni changamoto kubwa zinazo wakabili wanahabari hao wakimbizi anaongeza.

"Tulipowasili hapa mjini Goma tumeanza kupokea jumbe za kututisha kutoka watu tusio wafahamu,lakini kwa msaada wa vyama vinavyo tetea wanahabari tulionywa jinsi yakujiendesha na kufanya kazi ".

Kwa zaidi ya miaka miwili sasa mbali na kituo chake cha redio , Vianney Watsongo anasema kuwa hali hii imewanyima uhuru  wakujieleza wakati huu ambapo vita vinaendelea kusambaa.

"Ndio tumenyimwa uhuru wakujieleza sababu tukiwa na habari ya kutangaza kuna mara wakuu wanatunyooshea kidole kwamba tunaegemea upande wa waasi.  Kusalia kwenye maeneo yanayo dhibitiwa na waasi haimaanishi kwamba mwanahabari amekuwa upande wao ".

"Wanakuwa na matatizo mengi ikiwemo uhaba wa chakula hata nyumba zakulala,tunafanya jitihada ili kuwatolea huduma za dharura lakini tunachohitaji ni kuona siku moja amani imerudi ili warejee majumbani kwao " , anasema afisa mkuu wa chama kinacho kutetea uhuru wa vyombo vya habari mkoani kivu kaskazini, JED.

Baadhi ya vituo vya redio kwenye wilaya za masisi na Rutshuru vililazimika kufunga matangazo baada ya kukimbia vita kwa wanahabari walio elekea katika mji wa Goma.

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, lilitenga siku hii  miaka 31 iliyopita, ili kukumbusha umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na kuzikumbusha serikali kuheshimu haki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.