Pata taarifa kuu

DRC: Mafuriko yasababisha familia 28,000 kuhama makaazi yao Kalemie

Nchini DRC, serikali ya mkoa wa Tanganyika, kusini mashariki mwa nchi hatimaye inazungumza kuhusu maafa ya asili yanayoukumba mji wa Kalemie. Kwa mujibu wa waziri wa masuala ya kibinadamu wa mkoa huo, kaya 28,000 zilizopoteza makazi zimeathiriwa na kuongezeka kwa maji ya Ziwa Tanganyika zimetambuliwa. Anahakikisha kwamba serikali tayari imewapatishia hifadhi. 

Bandari ya Kalemie, Machi 22, 2018 huko Kalemie, kwenye mwambao wa magharibi wa Ziwa Tanganyika.
Bandari ya Kalemie, Machi 22, 2018 huko Kalemie, kwenye mwambao wa magharibi wa Ziwa Tanganyika. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara
01:40

DRC- Kalemie hali ya maisha ya waathiriwa 020524

Miongoni mwa waathiriwa, mamia kadhaa walipata hifadhi katika kijiji cha Mukuku karibu kilomita 4 kaskazini mwa mji wa Kalemie.

Waathiriwa wengine walihamia katika kijiji cha Katanika, magharibi mwa Kalemie. Baadhi wamejenga makazi ya muda, wengine wanaishi na familia zilizowapokea na kuwapa hifadhi. Hivi sasa,  familia 28,000 zimehamishwa na janga hili. Dieudonné Kabulo, kiongozi wa Tume ya kitaifa ya haki za binadamu, CNDH huko Kalemie anasema kuna dharura.

Maafa kama haya yanapotokea, ni Serikali ambayo inapaswa kuchukua hatua ili kukabiliana nayo na sio raia. Ni lazima iwahudumie wahanga,  ikibidi hata kujenga kambi ya waliohama maana inakuwa janga.

Kwa upande wake, Bob Morisho, waziri wa mkoa wa masuala ya kibinadamu, amesema  maeneo ya kuwahifadhi watu hao, yamepatikana na kwamba mazungumzo yanaendelea ili kuwaandalia misaada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.