Pata taarifa kuu

Amnesty International: Uhuru wa waandishi wa habari 'uko hatarini' Niger

Uhuru wa waandishi wa habari uko "hatarini" nchini Niger tangu mapinduzi ya kijeshi ambayo yalimpindua rais mteule Mohamed Bazoum mnamo mwezi Julai 2023, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limesema leo Ijumaa katika taarifa.

Amnesty International inalaani vitisho na kukamatwa kwa waandishi wa habari na mamlaka ya Niger.
Amnesty International inalaani vitisho na kukamatwa kwa waandishi wa habari na mamlaka ya Niger. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika hili la Haki za Binadamu linaandika kwamba "vitisho na kukamatwa kwa waandishi wa habari wanaofanya kazi kwenye mzozo" nchini Niger ambapo makundi ya wajihadi yametandaa kote nchini, huweka "uhuru wa waandishi wa habari hatarini". Amnesty pia inasisitiza kwamba "waandishi wa habari hawafanyi kazi yao vilivyo kwa kuogopa vitisho na ulipizaji kisasi".

"Dharau hii kwa haki ya uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari, na vile vile kazi ya waandishi wa habari, inajidhihirisha wakati ambao watu wanahitaji habari tu juu ya mzozo na majibu yanayotolewa na mamlaka ya mpito," amesema Samira Daoud, afisa wa Amnesty International katika ukanda wa Afrika Magharibi na Kati. Anaomba viongozi "waachilie waandishi wa habari waliokamatwa na kuwekwa kizuizini bila masharti ya kutumia haki yao ya uhuru wa kujieleza au kwa kutengeneza habari nyeti za masilahi ya umma".

Amnesty International inataja kukamatwa kwa Mkurugenzi wa Gazeti la kila siku la kibinafsi la Enquêteur, ambalo ni maarufu nchini Niger, akituhumiwa "kuhatarisha Ulinzi wa taifa" baada ya Gazeti lake kuchapisha makala "juu ya madai ya vifaa vya kunasa sauti vilivyowekwa na maafisa wa Urusi kwenye majengo ya serikali ". "Anakabiliwa na kifungo hadi miaka 10 jela," Amnesty International imesema. Shirika hili pia linataja kukamatwa, Aprili 13, kwa Ousmane Toudou, mwandishi wa habari na mshauri wa zamani wa mawasiliano kwa rais aliyeng'atuliwa mamlakani Mohamed Bazoum.

"Katika siku ambazo zilifuatia mapinduzi ya Julai 2023, Ousmane Toudou alikuwa ametoa wito kwa Wwnamocrats wote kupinga jeshi kuchukuwa madaraka katika chapisho lililosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii. Tangu kukamatwa kwake na vikosi vya usalama, "bado hajafikishwa mbele ya jaji ili aweze kusikilizwa, wakati kipindi cha polisi kumshikilia mtuhumiwa kisheria, kilichowekwa kwa siku 4, kilimalizika, "Amnesty imeandika

Shirika hili la Haki za Binadamu linabainisha kuwa anatakiwa kusikilizwa na "mahakama ya jeshi, licha ya vifungu vya sheria za kimataifa ambavyo vinadai kwamba mahakama ya jeshi inahukumu tu makosa ya kijeshi".

Niger imepoteza nafasi 26 (66)  kwenye orodha ya shirika la Waandishi wa Habari wasio na Mipaka (RSF) mwaka 2024 iliyotolewa leo Ijumaa kwenye hafla ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.