Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Mauritania: Nouakchott kwa mara nyingine tena yalaani mivutano kwenye mpaka wa Mali

Msemaji wa serikali ya Mauritania alitangaza Alhamisi hii kwamba mpaka na Mali si shwari na unakabiliwa na "mavuguvugu mengi kati ya makundi yenye silaha na jeshi la Mali". Alibainisha kuwa jeshi la Mauritania litawalinda raia wake nje, na pia ndani ya Mauritania. Wiki mbili zilizopita, waziri wa ulinzi wa Mauritania alikwenda Bamako kuomba maelezo kutoka kwa serikali ya mpito ya Mali baada ya "mashambulio ya mara kwa mara dhidi ya raia kadhaa wa Mauritania katika eneo la Mali".

Mwanajeshi wa Mauritania mwaka wa 2018. (Picha ya kielelezo)
Mwanajeshi wa Mauritania mwaka wa 2018. (Picha ya kielelezo) AFP - THOMAS SAMSON
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Nouakchott, LΓ©a Breuil

Msemaji wa serikali ya Mauritania Nani Ould Chrouga anathibitisha kuwa wanajeshi wa Mauritania wako tayari kikamilifu kutetea "uadilifu wa eneo la nchi". Kabla ya kuongeza kuwa "ukiukaji wowote wa hiari wa eneo la Mauritania, popote unapotoka, utakandamizwa na vikosi vya jeshi".

Nani Ould Chrougha pia alisisitiza umuhimu wa kuwalinda raia wa Mauritania kutoka nje ya nchi, akibainisha kuwa Mauritania inafuata utaratibu wa kimataifa unaohusu matukio yanayotokea nje ya mipaka.

Wiki mbili zilizopita, mkuu wa diplomasia ya Mauritania alimwita balozi wa Mali huko Nouakchott kupinga "mashambulio ya mara kwa mara dhidi ya raia wa Mauritania wasio na hatia na wasio na ulinzi ndani ya ardhi ya Mali".

Waziri wa Ulinzi wa Mauritania alikwenda Bamako kutafuta suluhu na kubainisha kwamba "kuhifadhi na kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni jukumu la pamoja".

Nani Ould Chrouga pia alifafanua kuwa usimamizi wa mpaka ulikuwa mgumu, hasa wakati "maeneo ya mpaka yanaingiliana kijiografia na watu". Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na jeshi, mkuu wa majeshi ya Mauritania kwa sasa anatembelea vitengo vya jeshi la Mauritania vilivyowekwa kwenye mpaka na Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.