Pata taarifa kuu

Rwanda yakanusha madai ya kushambulia kambi ya wakimbizi nchini DRC

Rwanda imekanusha madai ya Marekani kuwa, wanajeshi wake walishambulia kwa mabomu  kambi ya wakimbizi  ya Mugunga Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kusababisha vifo vya watu tisa siku ya Ijumaa asubuhi.

Rais wa Rwanda  Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya Rwanda inakuja baada ya Marekani kupitia Wizara ya Mambo ya nje, kulaani mashambulio hayo na kuwalaumu wanajeshi wa Rwanda na waasi wa M 23 kwa  kuhusika.

Msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, katika taarifa aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa X, amekanusha madai hayo na kuwatuhumu waasi wa FDLR na Wazalendo, aliosema wanaungwa mkono na serikali na jeshi la DRC kwa kurusha mabomu hayo.

Aidha, amesema wanajeshi wa Rwanda ni weledi na hawazi kuwalenga na kuwashambulia wakimbizi.

Kutokana na mashambulio hayo, rais Felix Thsisekedi ambaye anazuru barani Ulaya amesema anasitisha ziara yake nchini Hungary ili kurejea nyumbani, kushughulikia changamoto hiyo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alipokutana na rais Thsisekedi jijini Paris, aliitaka Rwanda kuacha kuwaunga mkono waasi wa M 23 na kuwaondoa wanajeshi wake mashariki wma DRC.

Haya yanajiri wakati huu waasi wa M 23 wanaoripotiwa kuungwa mkono na Rwanda, wakiendelea kuchukua maeneo kadhaa jimboni Kivu Kaskazini, wiki hii walifanikiwa kuudhibiti mji wenye utajiri wa madini wa Rubaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.