Pata taarifa kuu

Mali, Niger na Burkina Faso zimehitimisha mchakato wa kuundwa kwa muungano wao

Nchi za Mali, Niger na Burkina Faso ambazo zinaoongozwa na watawala wa kijeshi, zimetangaza kuhitimisha mipango ya kuundwa kwa muungano wao baada ya uhusiano kati ya mkoloni wao nchi ya Ufaransa kuingia doa.

Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka katika mataifa hayo matatu, Ijumaa ya wiki hii walikutana katika mji mkuu wa Niger, Niamey kuafikiana kuhusu uzinduzi wa muungano huo wa nchi za Sahel.
Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka katika mataifa hayo matatu, Ijumaa ya wiki hii walikutana katika mji mkuu wa Niger, Niamey kuafikiana kuhusu uzinduzi wa muungano huo wa nchi za Sahel. AFP - FANNY NOARO-KABRE
Matangazo ya kibiashara

Katika siku za hivi karibuni, mataifa hayo ya Afrika Magharibi yameonekana kuegemea upande wa nchi ya Urusi ambazo inasema itazisaidia kumaliza matatizo ya utovu wa usalama.

Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka katika mataifa hayo matatu, Ijumaa ya wiki hii walikutana katika mji mkuu wa Niger, Niamey kuafikiana kuhusu uzinduzi wa muungano huo wa nchi za Sahel, maarufu kama Confederation of the Alliance of Sahel States (AES).

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni wa Niger, Bakary Yaou Sangare, lengo kuu la mkutano huo ilikuwa ni kuangazia namna muungano huo utafanya kazi.

Nchi za Mali, Burkina Faso na Niger ambazo zinaoongozwa na jeshi zinataka kuunda muungano wao.
Nchi za Mali, Burkina Faso na Niger ambazo zinaoongozwa na jeshi zinataka kuunda muungano wao. © AFP - HAMA BOUREIMA

Aidha ameeleza kuwa jina hilo jipya litajadiliwa wakati wa mkutano wa viongozi wa mataifa hayo bila kutaja tarehe ambayo watakutana.

Kwa upande wake, Waziri wa mambo ya nje wa Mali, Abdoulaye Diop baada ya kukutana na rais wa kijeshi wa Niger Abdourahamane Tiani, alisema ni rasimi sasa muungano mpya umezinduliwa.

Burkina Faso nayo iliwakilishwa kwenye mkutano huo na waziri wake wa mambo ya kigeni Karamoko Jean-Marie Traore.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za Niger, Burkina Faso na Mali.
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za Niger, Burkina Faso na Mali. © AFPTV

Ukanda wa Sahel umekuwa ukikabiliwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa wanajihadi kwa miaka kadhaa sasa, nchi za ukanda huo zikiituhumu Ufaransa kwa kushindwa kuyakabili makundi yenye silaha.

Mwezi Januari mwaka huu, nchi za Mali, Niger na Burkina Faso zilitangaza kuwa zinajiondoa katika muungano wa ECOWAS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.