Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Marekani: Wanafunzi kadhaa wakamatwa wakiandamana kupinga vita Gaza

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Columbia kilichopo jijini New York, wamemakamatwa na polisi baada kuanzisha maandamano ya kulaani vita vinavyoendelea kwenye ukanda wa Gaza.

Polisi wanatumia gari linaloitwa "The Bear" kuingia kwenye Ukumbi wa Hamilton kutoka kwenye barabara ya umma, uliokuwa umekaliwa na waandamanaji, huku maafisa wengine wakiingia katika chuo kikuu cha Columbia, New York, Marekani, Aprili 30, 2024.
Polisi wanatumia gari linaloitwa "The Bear" kuingia kwenye Ukumbi wa Hamilton kutoka kwenye barabara ya umma, uliokuwa umekaliwa na waandamanaji, huku maafisa wengine wakiingia katika chuo kikuu cha Columbia, New York, Marekani, Aprili 30, 2024. REUTERS - Caitlin Ochs
Matangazo ya kibiashara

Polisi wamewamia wafunzi hao waliokuwa wamejifungia kwenye ukumbi wa Hamilton, kwenye chuo na kuwakamata.

Kabla ya hatua hiyo, mamia ya wanafunzi walikuwa wafunga barabara za kuingia kwenye chuo hicho, na kuapa kuendeleza maandamano hayo,; hadi pale mashambulio kwenye ukanda wa Gaza, yatakapokoma.

Uongozi wa Chuo hicho, umesema waandamanaji waliovamia ukumbi huo sio wanafunzi wa taasisi hiyo ya elimu na hivyo kuomba maafisa wa usalama kusaidia kuwaondoa.

Aidha, wanafunzi walioingia kwneye ukumbi huo wametishiwa kufukuzwa chuoni, huku rais Joe Biden alilaani kile alichosema maandamano yasiyokuwa na amani baada ya kushuhudiwa uharibifu na makabiliano na maafisa wa polisi.

Mbali na Chuo Kikuu cha Columbia, wafunzi kwenye vyuo vikuu vingine nchini Marekani na hata Ufaransa kwa siku kadhaa zilizopita, wamekuwa wakiandamana kuwaunga mkono Wapalestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.