Pata taarifa kuu
SIASA-USALAMA

Haiti: Baraza la Mpito lamchagua Edgard Leblanc Fils kama rais

Baraza jipya la Rais la Mpito nchini Haiti, lililoundwa baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, limemchagua Jumanne hii, Aprili 30, mwanasiasa Edgard Leblanc Fils kuwa mwenyekiti wa baraza hilo. Tangazo hilo limetolewa wakati wa hafla rasmi iliyotangazwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Edgard Leblanc fils, mkuu mpya wa Baraza la Mpito la Rais nchini Haiti, wakati wa hafla mjini Port-au-Price, Jumanne hii Aprili 30, 2024.
Edgard Leblanc fils, mkuu mpya wa Baraza la Mpito la Rais nchini Haiti, wakati wa hafla mjini Port-au-Price, Jumanne hii Aprili 30, 2024. AFP - CLARENS SIFFROY
Matangazo ya kibiashara

Edgar Leblanc Fils atakuwa na jukumu la kuratibu ndani ya Baraza, lililotawazwa wiki iliyopita, na kazi nzito ya kujaribu kurejesha utulivu wa umma katika nchi iliyoharibiwa na magenge yenye silaha.

Wajumbe wengi wa baraza hilo pia wamependekeza jina la Fritz Bélizaire kwa wadhifa wa Waziri Mkuu, Frinel Joseph, mmoja wa wajumbe wawili wasiopiga kura wa Baraza, alitangaza kwa watazamaji, akiahidi "maelezo mengi zaidi" baadaye.

Rais mpya wa Baraza amechaguliwa kufuatia makubaliano kati ya wajumbe saba wenye haki ya kupiga kura ndani ya chombo hicho, na sio uchaguzi wa ndani kama ulivyopangwa. "Leo asubuhi, tuliweka masanduku ya kupigia kura, kibanda cha kupigia kura bila malipo," aliomba msamaha Frinel Joseph. "Lakini zaidi ya yote, kilicho muhimu ni kwamba wengi waliondolrwa. Inaweza kutokea kwamba kuna mabadiliko ya mpango, lakini ni muhimu hasa [...] kwamba mabadiliko ya mpango hutoa matokeo sawa.

“Na matokeo yake ni kwamba, mabibi na mabwana, leo Jumanne, Aprili 30, tunaye rais maarufu ndani ya Baraza la Rais, ambaye ataratibu Baraza kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa kati ya wadau mbalimbali ” ameongeza.

Ilichukua majuma kadhaa ya mazungumzo magumu, yakiwa na mabadiliko, ili Barazaliweze kuundwa. Sababu ni kutoelewana kati ya vyama vya siasa na wadau wengine, lakini pia na serikali inayomaliza muda wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.