Pata taarifa kuu

Maandamano ya wanafunzi dhidi ya vita Gaza yanaendelea Marekani na kuenea hadi Canada

Maandamano ya kuunga mkono Palestina katika vyuo vikuu unaendelea nchini Marekani. Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mfano kwenye kampasi ya Chuo Kikuu cha George Washington huko Washington, baada ya polisi kusambaratisha mikusanyiko huko Columbia na UCLA. Uhamasishaji wa kukalia kamapasi za vyuo vikuu sasa zinaenea kote Canada.

Maandamano dhidi ya vita huko Gaza kwenye kampasi ya Chuo Kikuu cha George Washington, Washington, Mei 3, 2024.
Maandamano dhidi ya vita huko Gaza kwenye kampasi ya Chuo Kikuu cha George Washington, Washington, Mei 3, 2024. AP - Susan Walsh
Matangazo ya kibiashara

Utulivu unatawala katika bustani ya Chuo Kikuu cha George Washington mjini Washington, chini ya kilomita moja kutoka Ikulu ya Marekani. Hakuna nyimbo, hakuna ngoma au kelele kupitia vipaza sauti, lakini katika siku chache, mikusanyiko imeongezeka. Sasa umati wa wanafunzi wako mitaani kwenye barabara ambayo imefungwa kwa usafiri wa magari.

Polisi hawana vifaa vyao vya kutuliza ghasia. Wengine hata huvuta sigara. Tuko mbali sana na mvutano na vurugu zinazoonekana huko New York na Los Angeles, amesema mmoja wa wanafunzi. Picha hizi pia ziliwashtua wanafunzi wanaoandamana kama Kayla.

"Inasikitisha sana," amesema, "kuona kwamba katika visa vingine viongozi, watu walioapa kutulinda, wanawatendea wanafunzi wetu ukatili au hawafanyi chochote kuwalinda. Na nadhani hiyo inaonyesha tu ushirikiano wa Marekani katika ukandamizaji na katika kazi hii. Hii inaonyesha kwamba vyuo vikuu vyetu vinahusishwa na mauaji haya ya kimbari, na kwamba wanafadhili kikamilifu, wako tayari kuwakandamiza na kuwashambulia wanafunzi wao wenyewe kwa kutotimiza matakwa yetu. "

Miongoni mwa matakwa hayo, kuna hasa kuachwa kwa uhusiano wa kifedha kati ya chuo kikuu na makampuni ambayo waandamanaji wanaona kuwa yanashiriki katika vita huko Gaza. Wanaijadili katika warsha zilizoandaliwa kambini. Kambi ambayo chuo kikuu kimeiomba polisi kuivunja. Lakini hadi sasa, meya wa Washington anapinga hilo.

Kambi sita katika vyuo vikuu vya Canada

Harakati hizi za uvamizi wa kampasi za kupinga uvamizi wa Israeli huko Gaza sasa zinaenea hadi Canada, ambapo kuna kambi sita kwenye uwanja wa chuo kikuu. Kwa sasa, hakuna iliyobomolewa na polisi, ambao hata hivyo wanatoa ulinzi wa eneo hilo, anaripoti mwandishi wetu huko Quebec, Pascale Guéricolas.

Sasa imepita wiki moja tangu wanafunzi wajenge takriban mahema mia moja kwenye kampasi ya Chuo Kikuu cha McGill kinachozungumza Kiingereza huko Montreal. Waandamanaji hao wanaitaka taasisi hii kuondoa uwekezaji wake katika makampuni ya silaha yanayohusika na mzozo wa Gaza.

Kwa mujibu wa Safia Chabi, mwanafunzi ambaye anaunga mkono hoja ya Palestina, majibu kutoka kwa wasimamizi wa chuo kikuu bado hayatoshi: "Kitu pekee ambacho mkuu wa chuo kikuu aliwaahidi wanafunzi wa McGill ni kwamba watafanya jukwaa la kujadili masuala haya baada ya kuvunjwa kwa kambi. Hakika, wanafunzi hawatakubali hilo kamwe. "

Baada ya Montreal, wanafunzi pia wanahamasishwa katika Chuo Kikuu cha Toronto ambapo kuna takriban mahema sitini. Jambo lile lile huko Vancouver, kama tu huko Ottawa. Wanafunzi wa chuo kikuu hiki wanaomba hasa kujitenga na benki ya Canada ambayo imewekeza katika kampuni ya silaha ya Israel.

Wasimamizi wa chuo kikuu kwa sasa wanaangalia hali hiyo, pamoja na polisi. Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amebainisha kuwa vyuo vikuu ni mahali pa mijadala, lakini kwamba kila mtu lazima ajisikie salama hapo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.