Pata taarifa kuu

Donald Trump apatikana na hatia kwa kutoa maoni juu ya kesi yake kwenye mitandao ya kijamii

Kesi ya jinai ya Donald Trump huko New York inaendelea kwa wiki kadhaa. Rais huyo wa zamani wa Marekani anatuhumiwa kuficha malipo yaliyokusudiwa kununua ukimya wa Stormy Daniels, nyota wa zamani wa picha za ngono yaani ponografia, kabla tu ya kuchaguliwa mwaka wa 2016. Donald Trump tayari amepata hatia ya kwanza kwa kudharau mahakama. Na hapo pia, ni suala la ukimya.

Donald Trump akitoka nje ya chumba cha mahakama iliyosikiliza kesi yake katika Mahakama ya Jinai ya Manhattan, Jumanne, Aprili 30, 2024, New York.
Donald Trump akitoka nje ya chumba cha mahakama iliyosikiliza kesi yake katika Mahakama ya Jinai ya Manhattan, Jumanne, Aprili 30, 2024, New York. AP - Curtis Means
Matangazo ya kibiashara

Faini ya dola elfu tisa: hivi ndivyo Donald Trump lazima alipe kwa kutoheshimu "Gag order", agizo la kunyamazisha lililowekwa kabla ya kuanza kwa kesi na Jaji Merchan. Mshtakiwa alilazimika kujiepusha na maoni yoyote juu ya mashahidi, haswa wakili wake Michael Cohen au mwigizaji wa zamani Stormy Daniels na juu ya washiriki wa majaji na mahakama.

Lakini Donald Trump alitaka kujaribu marufuku, haswa kwa kusambaza machapisho kwenye mitandao ya kijamii ambayo yeye hakuwa mhusika. Kwa mujibu wa jaji, kurusha tena machapisho kwenye mitandao ya kijamii kunaidhinisha na anamhukumu Donal Trump hadi faini ya juu zaidi ya dola1,000 kwa kila kosa kati ya tisa alilobaini. Kwa onyo: ikiwa itatokea tena, hukumu inaweza kuwa kifungo jela.

Kwa hivyo Donald Trump alitii kwa kufuta machapisho tisa yanayozungumziwa, lakini kwa neema mbaya kwani, katika moja wapo iliyochapishwa kwenye mtandao wake wa kijamii wa kibinafsi, anamshutumu jaji huyo kwa kumnyima haki yake ya kujieleza na kumfanya yeye pekee aliye mgombea urais kufedheheshwa katika historia.

Ni kwa kesi hiyo ya ukimya ambapo rais huyo wa zamani, Jumanne hii, Aprili 30, alilazimika kusikiliza ushahidi wa wakili wa nyota wa zamani wa picha za ngono ambaye alidai kuwa Donald Trump alikuwa na uhusiano wa nje ya ndoa naye. Kesi yake ilikuwa imenunuliwa ili kuzikwa na marafiki wa rais huyo wa zamani. Sasa inasikilizwa hadharani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.