Pata taarifa kuu

Watu kadhaa wafariki kusini mwa Brazili kutokana na hali mbaya ya hewa

Watu 32 wamefariki kusini mwa Brazil kutokana na hali mbaya ya hewa kusini mwa Brazili, watu wengine wengi wamejeruhiwa na maelfu hawana makazi, wakati mvua kubwa inaendelea kunyesha. Mkoa huo ulikumbwa na mafuriko makubwa mwezi wa Septemba mwaka uliyopita.

Wakazi wa Kisiwa cha Pintada wakihamishwa kutoka eneo lililokumbwa na mafuriko huko Porto Alegre katika jimbo la Rio Grande do Sul, Mei 2, 2024.
Wakazi wa Kisiwa cha Pintada wakihamishwa kutoka eneo lililokumbwa na mafuriko huko Porto Alegre katika jimbo la Rio Grande do Sul, Mei 2, 2024. AFP - CESAR LOPEZ
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu katika Sao Paulo, Martin Bernard

Bwawa limevunja kingo zake na madaraja yamedondoka kutokana na uzito wa maji. Jimbo la Rio Grande do Sul limekumbwa tena tangu mwanzoni mwa juma kutokana na mvua kubwa inayonyesha na kusababisha mito kufurika maji na kuharibu eneo hilo. Wakazi wa maeneo hatarishi ndio walio hatarini zaidi, kama vile wazee.

Timu za uokoaji za ndani zimezidiwa haraka na ukubwa wa hali hiyo. Rais wa Brazil Lula alizuru eneo hilo siku ya Alhamisi. Aliweka uwezo wote wa serikali kwa gavana wa eneo hilo, ambaye alikiri kwamba haiwezekani kabisa kusaidia kila mtu katika hali ya sasa.

Matukio ya hali ya hewa kali yanarudiwa kwa mzunguko mkubwa. Eneo hilo, ambalo halipo katika eneo la kitropiki, lilikumbwa na kimbunga kikali mnamo mwezi wa Septemba mwaka uliypita. Idadi ya waliokufa iliongezeka hadi 53. Kosa ni El Niño, lakini pia mabadiliko ya hali ya hewa, kulingana na wataalam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.