Pata taarifa kuu

Brazili: Baada ya wimbi la joto, kimbunga chasababisha vifo kusini-mashariki

Baada ya halijoto iliyorekodiwa wiki hii, dhoruba kali ilipiga Brazil siku ya Ijumaa Machi 22. Katika eneo la Rio de Janeiro, watu tisa wamefariki kutokana na hali mbaya ya hewa. Idadi ambayo kwa mwakati wowote inaweza kuongezeka zaidi, kwa sababu hali inaendelea kuwa mbaya wikendi hii.

Hisia za mkazi wa Petropolis, Brazili mnamo Machi 23, 2024, wakati waokoaji walipompata msichana wa miaka 4 akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka baada ya kimbunga kikali.
Hisia za mkazi wa Petropolis, Brazili mnamo Machi 23, 2024, wakati waokoaji walipompata msichana wa miaka 4 akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka baada ya kimbunga kikali. AP - Bruna Prado
Matangazo ya kibiashara

Mvua kubwa zilinyesha kwa zaidi ya saa 24 katika mji wa Petropolis, mji wa kitalii ulioko kando ya mlima kilomita 70 kutoka Rio de Janeiro. Mvua zilizorekodiwa ziligeuza Mto Quitandinha kuwa kimbunga chenye nguvu ambacho kilipasua kingo zake na kusomba kila kitu kilichokuwa wakati kilipokuwa kikipita.

Madaraja yalibomolewa, barabara zilijaa maji na maporomoko ya udongo yalifukia majengo ya makazi ya ghorofa nyingi. Vikosi vya polisi na jeshi vilitumwa katika maeneo mbalimbali kusaidia waokoaji kupata manusura.

Baada ya joto la kipekee, huku halijoto ikifika katika kiwango cha zaidi ya 60° wiki hii mjini Rio, kuwasili kwa eneo baridi katika eneo la Karibea kunasababisha hali hii ya kimbunga kikali. Hii sio mara ya kwanza kwa Petropolis kukumbwa na janga la asili: mnamo 2023, watu 180 waliuawa mnamo mwezi wa Februari, na wengine 150 mnamo mwezi wa Novemba, wakati wa mafuriko kama hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.