Pata taarifa kuu

Argentina inaziomba Pakistan, Sri Lanka kumkamata waziri wa mambo ya ndani wa Iran

Serikali ya Argentina siku ya Jumanne, Aprili 23, iliziomba Pakistan na Sri Lanka kumkamata Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Ahmad Vahidi, aliyekuwa akitafutwa kwa shambulio dhidi ya mfuko wa pamoja wa Kiyahudi wa Amia huko Buenos Aires mwaka 1994. Anayechukuliwa kuwa muasisi wa shambulio kubwa zaidi la kihistoria nchini humo, kwa sasa anazuru nchi hizi mbili.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Ahmad Vahidi akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran mnamo Machi 4, 2024.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran Ahmad Vahidi akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran mnamo Machi 4, 2024. © Atta Kenare / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Argentina inataka kukamatwa kwa ngazi ya kimataifa kwa wale waliohusika na shambulio la bomu la mwaka 1994 la AMIA (Jumuiya ya Wayahudi kutoka Argentina), ambalo lilisababisha vifo vya watu 85, na ambao wanaendelea kushikilia nyadhifa zao serikalini bila kuadhibiwa kabisa," Waziri wa Mambo ya Nje wa Argentina iimeandika katika taarifa.

“Mmoja wao ni Ahmad Vahidi, anayedaiwa na mahakama ya Argentina kuwa mmoja wa waliohusika na shambulio dhidi ya AMIA. Mtu huyu kwa sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ni sehemu ya ujumbe wa serikali unaotembelea Pakistan na Sri Lanka siku hizi,” taarifa hiyo inaendelea.

"Argentina imeomba serikali za Pakistan na Sri Lanka kumkamata kwa mujibu wa taratibu zilizotolewa na Interpol," taarifa ya wizara inaongeza.

Jenerali Vahidi amekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani tangu 2021, baada ya kuwa Waziri wa Ulinzi. Wakati wa shambulio la Buenos Aires, aliongoza Kikosi cha Quds, kitengo cha operesheni za siri ndani ya Walinzi wa Mapinduzi, jeshi la itikadi kali la utawala wa Iran.

Shambulio la AMIA la Julai 18, 1994 lilihusishwa na mahakama za Argentina na Israel na utawala wa Iran na vuguvugu la Kishia la Lebanon la Hezbollah, mshirika wake. Iran imekanusha kuhusika na mara zote ilikataa kuruhusu maafisa wanane wa zamani waliofunguliwa mashtaka na mahakama za Argentina, akiwemo Jenerali Vahidi na Rais wa zamani Ali Rasfanjani, kuhojiwa.

Argentina ina jumuiya kubwa zaidi ya Wyahudi katika Amerika ya Kusini, wakifikia idadi ya 300,000.

Kabla ya AMIA, ubalozi wa Israel mjini Buenos Aires ulilengwa na shambulio mwaka 1992 ambalo lilisababisha vifo vya watu 29 na 200 kujeruhiwa. Iran pia ililaumiwa.

Mnamo mwaka 2013, rais wa Argentina wa wakati huo Cristina Kirchner alitia saini mkataba wa itifaki na Iran kuunda "tume ya ukweli" kuchunguza shambulio hilo. Itifaki hiyo pia ilitaka kuwezesha waendesha mashtaka wa Argentina kusafiri nje ya nchi kuwahoji washtakiwa.

Mkataba huu uliidhinishwa na Bunge la Argentina, lakini kamwe na Bunge la Iran. Alikashifiwa na viongozi wa jumuiya ya Wayahudi nchini Argentina, ambao walimshutumu Cristina Kirchner kwa kuwaficha wahusika wa shambulio hilo. Uchunguzi wa mahakama ulifunguliwa kuhusu suala hili mwaka wa 2015, hata hivyo, ulimalizika na kufutwa kwa kesi hiyo mwaka wa 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.