Pata taarifa kuu

Blinken anafanya mazungumzo na Riyadh kwa ajili ya kufufua uhusiano na Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anatarajiwa nchini Israel tarehe 30 Aprili. Alianza ziara mpya ya Mashariki ya Kati ili kuendeleza usitishaji vita wa kutetea amani katika eneo la Palestina. Jumatatu tarehe 29, alikuwa Saudi Arabia ambako alitoa wito wa kuwepo kwa umoja wa kikanda dhidi ya Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ahudhuria Mkutano wa Pamoja wa Mawaziri wa GCC-U.S. Ushirikiano wa kimkakati wa kujadili majanga ya kibinadamu yanayokabili Gaza, Riyadh, Saudi Arabia, Aprili 29, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ahudhuria Mkutano wa Pamoja wa Mawaziri wa GCC-U.S. Ushirikiano wa kimkakati wa kujadili majanga ya kibinadamu yanayokabili Gaza, Riyadh, Saudi Arabia, Aprili 29, 2024. REUTERS - Evelyn Hockstein
Matangazo ya kibiashara

Antony Blinken alitangaza kufanyika katika wiki zijazo kwa majadiliano na nchi sita za Ghuba juu ya ushirikiano wa ulinzi wa anga na makombora na juu ya kuimarisha usalama wa baharini. Kulingana na Antony Blinken, ni muhimu kukuza uelewa wa kikanda ikiwa ni pamoja na Israeli. Waziri wa Mambo ya Nje pia alitangaza kuwa Marekani iko tayari kutoa dhamana ya usalama ya Saudi Arabia ikiwa itarekebisha uhusiano na Israel.

Riyadh ilitangaza miezi miwili iliyopita kwamba hakutakuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Israel hadi taifa la Palestina litambuliwe. Hili pia ndilo suluhisho ambalo Washington inaunga mkono leo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.