Pata taarifa kuu

Marekani yataka Misri na Qatar kuhakikisha mateka wa Israel wanaachiwa huru mara moja

Rais wa Marekani Joe Biden, amewaambia viongozi wenzake wa Misri na Qatar kutumia mbinu zote kuhakikisha kuwa, mateka wanaoshikiliwa na Hamas wanaachiwa huru wakati huu mazungumzo kusitisha vita kati ya kundi hilo na Israeli yakiendelea.

Rais wa Marekani Joe Biden.
Rais wa Marekani Joe Biden. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Wito huu unakuja, wakati wajumbe kutoka Marekani, Qatar na Misri kwa miezi kadhaa sasa wakiongoza majadiliano kujaribu kupata mkataba wa kusitisha vita vilivyoanza Oktoba 7 mwaka uliopita.

Jana, wawawakilishi wa Misri, Qatar na Hamas walikutana jijini Cairo kwa majadiliano zaidi na sasa uongozi wa Hamas, unatarajiwa kutoa uamuzi wao kuhusu mapendekezo ya kusitisha vita.

Wakati hayo yakijiri, ndege za kivita za Israeli zimeendeleza mashambulio kwenye ukanda wa Gaza, ambapo kuanzia Jumatatu usiku, watu zaidi ya 30 wameuawa, wakiwemo watatu waliokuwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Nuseirat.

Katika hatua nyingine, afisa wa serikali ya Marekani kutoka Wizara ya Mambo ya nje, amesema Mahakama ya Kimataifa ya ICC haina uwezo wa kuishinikiza Israel kusitisha mashambuluo yake kwenye ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.