Pata taarifa kuu

Togo: Kampeni zinaendelea kuelekea uchaguzi wa wabunge wiki ijayo

Kampeni za uchaguzi zinaendelea nchini Togo, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa wabunge na wa kikanda Jumatatu ijayo nchini humo.

Bango la rais Faure Gnassingbe, mgombea urais kuipitia (Union for the Republic), jijini Lome, Togo, Februari 19, 2020. Picha Februari 19, 2020. REUTERS/Luc Gnago/File Photo
Bango la rais Faure Gnassingbe, mgombea urais kuipitia (Union for the Republic), jijini Lome, Togo, Februari 19, 2020. Picha Februari 19, 2020. REUTERS/Luc Gnago/File Photo © Reuters / Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Ni kampeni ambazo zinafanyika baada ya mwishoni mwa juma lililopita, wabunge kuipigia kura katiba mpya yenye utata ambayo sasa italiondoa taifa kutoka utawala wa rais hadi wa bunge.

Rais Faure Gnassingbé ana siku kumi na tano kuitangaza rasmi, ambapo sasa rais atachaguliwa na wabunge na sio wananchi, hatua ambayo hata hivyo imekosolewa vikali na wapinzani nchini humo.

Soma piaTogo: Ecowas kujaribu kupata suluhu ya kisiasa baada ya mabadiliko ya katiba

Hata hivyo licha ya maandalizi ya kura mbili kuendelea, tume ya uchaguzi huko Togo imelikataa ombi la kanisa Katoliki la kupeleka waangalizi na sasa imeendelea kukamilisha zoezi la kusafirisha vifaa vya kupigia kura.

Uchaguzi wa wabunge huko Togo utafanyika tarehe 29 mwezi huu wa Aprili mwaka huu, na baada ya kutangazwa rasmi kwa katiba mpya, bunge hili litakuwa na mamlaka ya kumchagua rais na sio tena wananchi.

RFI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.