Pata taarifa kuu

Rais mteule wa Indonesia Prabowo Subianto ahusishwa na ukatili wa siku za nyuma

Tangu kutangazwa rasmi kwa ushindi wake Jumatano Machi 20, Rais mteule wa Indonesia Prabowo Subianto amepokea simu na jumbe kutoka kwa viongozi kadhaa duniani. Jirani yake, Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim, alikuwa wa kwanza kumpongeza. Ijumaa, Joe Biden naye alimpongeza kwa simu. Lakini Bw. Subianto, waziri wa ulinzi wa sasa, ni mtu anayehusishwa kwa ukatili uliyotekelezwa katika siku za nyuma.

Rais Mteule wa Indonesia Prabowo Subianto, mjini Jakarta mnamo Machi 20, 2024, muda mfupi baada ya ushindi wake kuthibitishwa na Tume ya Uchaguzi Mkuu.
Rais Mteule wa Indonesia Prabowo Subianto, mjini Jakarta mnamo Machi 20, 2024, muda mfupi baada ya ushindi wake kuthibitishwa na Tume ya Uchaguzi Mkuu. AFP - BAY ISMOYO
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu katika kanda, Juliette Pietraszewski

Mkwe wa zamani wa dikteta Suharto, na mkuu wa zamani wa kikosi maalum, Prabowo Subianto alishutumiwa namashirika ya haki za binadamu, na maafisa wake wa zamani, kwa kuagiza kutekwa nyara kwa wanaharakati wanaounga mkono demokrasia katika miaka ya 1990.

Mwanajeshi huyu wa zamani pia alinyimwa visa na Marekani na Australia kwa muda mrefu. anahusishwa kwa mauaji ya wanaharakati wanaounga mkono demokrasia. Mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali hayafichi wasiwasi wao.

Ikiwa mtu husika alikana shutuma hizi na hajawahi kufunguliwa mashtaka, baadhi ya mashirika yanazua maswali kuhusu mustakabali wa nchi hii ya tatu inaoimarisha demokrasia duniani.

"Kwa bahati mbaya, Indonesia itaongozwa na mtu ambaye rekodi yake ya haki za binadamu ina utata, na kuibua wasiwasi kuhusu kujitolea kwake kwa haki na uwajibikaji," anasema Usman Hamid, mkurugenzi wa shirika la haki za binadamu la Amnesty International nchini Indonesia.

Uchunguzi ulioshirikiwa na Phil Robertson, mkurugenzi wa Human shirika la haki za binadamu la Rights Watch barani Asia. "Prabowo ni mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu," amesema, "ambaye alisimamia kutoweka kwa lazima kwa wanafunzi wanaounga mkono demokrasia huko Jakarta mnamo mwaka 1998 na ambaye aliongoza mauaji ya raia huko Timor Mashariki wakati nchi hiyo ikihangaika kupata uhuru wake kutoka kwa Indonesia. Nafasi yake ni jela kwa makosa haya, sio ikulu ya rais wa Indonesia. Demokrasia ya Indonesia inakaribia kukabiliana na changamoto kubwa zaidi tangu kupinduliwa kwa Suharto. Washirika wakuu wa Indonesia lazima sasa wafanye mazungumzo magumu na Prabowo na kumwambia kwamba kurejea kwa ukandamizaji wa kisiasa kutamgharimu yeye na Indonesia katika masuala ya biashara, misaada na hata vikwazo vinavyowezekana. "

Prabowo Subianto anatarajiwa kuapishwa kama rais mpya wa Indonesia mnamo Oktoba 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.