Pata taarifa kuu

UNHCR yahofia makumi ya vifo baada ya boti iliyokuwa imebeba wakimbizi wa Rohingya kuzama

Shirika la Umoja wa Mataifa linalouhudumia wakimbizi (UNHCR) limesema leo Ijumaa Machi 22 kwamba linahofia makumi ya vifo katika ajali ya boti iliyozama kwenye pwani ya Indonesia. Boti hiyo ilikuwa imebeba wakimbizi wa Rohingya, sabini na tano kati yao waliokolewa.

Wakimbizi wa Rohingya waliokolewa kutoka kwa boti yao iliyopinduka wakiingzwa ndani ya meli ya shirika la kitaifa la Utafutaji na Uokoaji karibu na Aceh Magharibi, Indonesia, Alhamisi, Machi 21, 2024. Boti ya mbao iliyokuwa imebeba makumi ya Waislamu wa Rohingya ilizama kwenye pwani ya kaskazini mwa Indonesia siku ya Jumatano, kulingana na wavuvi wa ndani.
Wakimbizi wa Rohingya waliokolewa kutoka kwa boti yao iliyopinduka wakiingzwa ndani ya meli ya shirika la kitaifa la Utafutaji na Uokoaji karibu na Aceh Magharibi, Indonesia, Alhamisi, Machi 21, 2024. Boti ya mbao iliyokuwa imebeba makumi ya Waislamu wa Rohingya ilizama kwenye pwani ya kaskazini mwa Indonesia siku ya Jumatano, kulingana na wavuvi wa ndani. © Reza Saifullah / AP
Matangazo ya kibiashara

Boti iliyokuwa imebeba makumi ya wakimbizi wa Rohingya, Waislamu walio wachache wanaoteswa huko Burma, ilipinduka siku ya Jumatano usiku. Watu sabini na watano waliokolewa. Shirika la Umoja wa Mataifa linalodumia wakimbizi linahofia makumi ya vifo.

Hata hivyo, kulingana na walionusurika, karibu watu mia moja na hamsini walikuwa kwenye boti hili, lakini takwimu hii haikuweza kuthibitishwa. Katika taarifa ya pamoja, UNHCR na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) wamesema "wameshtushwa na kusikitishwa sana na hali hiyo". "Kama [takwimu] itathibitishwa, itakuwa hasara kubwa kwa vifo hivi vya watu kufikia sasa mwaka huu," inaeleza taarifa kwa vyombo vya habari.

Idara ya huduma za dharura ya Indonesia imetangaza siku ya Ijumaa kwamba wamemaliza zoezi la kutafuta manusura wengine. "Zoezi la kutafuta manusura wengine lilimalizika siku ya Alhamisi," amesema Muhammad Fathur Rachman, afisa wa shirika la utafutaji na uokoaji katika eneo hilo huko Aceh, kwenye ncha ya magharibi ya kisiwa kikubwa cha Sumatra. “Hatujapokea taarifa zozote za ziada kuhusu watu waliotoweka, na hakuna orodha ya abiriawaliokuwa wakisafiri kwa boti. Kulingana na uchambuzi wetu, boti [halingeweza] kubeba watu mia moja na hamsini,” ameongeza.

Wakimbizi wa Rohingya waliokolewa kutoka kwa boti yao iliyopinduka wakiingzwa ndani ya meli ya shirika la kitaifa la Utafutaji na Uokoaji karibu na Aceh Magharibi, Indonesia, Alhamisi, Machi 21, 2024. Boti ya mbao iliyokuwa imebeba makumi ya Waislamu wa Rohingya ilizama kwenye pwani ya kaskazini mwa Indonesia siku ya Jumatano, kulingana na wavuvi wa ndani.
Wakimbizi wa Rohingya waliokolewa kutoka kwa boti yao iliyopinduka wakiingzwa ndani ya meli ya shirika la kitaifa la Utafutaji na Uokoaji karibu na Aceh Magharibi, Indonesia, Alhamisi, Machi 21, 2024. Boti ya mbao iliyokuwa imebeba makumi ya Waislamu wa Rohingya ilizama kwenye pwani ya kaskazini mwa Indonesia siku ya Jumatano, kulingana na wavuvi wa ndani. © Reza Saifullah / AP

Kuchoka na kiwewe

Siku ya Alhamisi, meli ya uokoaji iliwachukua wakimbizi sitini na tisa ambao walikuwa wamenusurika kwa saa nyingi, chini ya jua kali, wakiwa wameng'ang'ania sehemu ya juu ya boti ya uvuvi kilomita 30 kutoka pwani. Miongoni mwao, watoto tisa, wanawake kumi na wanane na wanaume arobaini na wawili.

"Walionekana wamechoka na wamepatwa na kiwewe. Nyuso za wanawake hao zilikuwa nyekundu, zilichomwa na jua,” ameeleza mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP aliyekuwa kwenye meli ya uokoaji. Kwa hofu, baadhi ya wanaume walijaribu kuruka ndani ya mashua iliyokuja kuwachukua, kabla ya waokoaji na baadhi ya wenzao kuwatuliza.

Wakimbizi hawa, kutoka jamii ya Waislamu walio wachache wanaoteswa nchini Burma, walikuwa wamenusurika kwa ajali mbili: meli ilitotengenezwa kwa mbao iliyowabeba kutoka Bangladesh ilipinduka siku ya Jumatano, kisha boti la wavuvi lililokuja kuwaokoa likapinduka pia.

Wanane wamelazwa hospitalini

Wakimbizi sita wa kwanza waliokolewa siku ya Jumatano na wavuvi. Angalau wanane wa walionusurika, waliopungukiwa na maji mwilini na wagonjwa, walilazwa hospitalini. Wengine walipelekwa kwenye kituo cha makazi ya muda - jengo la zamani la shirik la Msalaba Mwekundu - katika kijiji kilicho karibu na Maulaboh, mji mkuu katika wilaya ya Aceh Magharibi. Kuwasili kwao kumezua maandamano kutoka kwa baadhi ya wakazi, ambao wana mtazamo hafifu wa kuwasili mara kwa mara kwa wakimbizi hao wanaodaiwa kula rasilimali zao ambazo tayari ni duni.

Tangu mwezi wa Novemba mwaka jana, mamia ya Warohingya wamekimbia kambi wanazoishi nchini Bangladesh hadi kufikia jimbo la Aceh kwa njia ya bahari, wakitumia boti. Kulingana na manusura wa ajali hiyo ya boti, walinuia kufika pwani ya Thailand lakini hatimaye walielekea Banda Aceh baada ya kurudishwa nyuma na Thailand.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.