Watu 19 wafariki baada ya barabara kuu kuporomoka kusini mwa China
Takriban watu 19 wamefariki baada ya barabara kuu kuporomoka katika jimbo la Guangdong kusini mwa China leo Jumatano, vyombo vya habari vya serikali vimesema.
Imechapishwa:
Magari 18 "yalinaswa" kutokana na kuporomoka kwa barabara kuu hiyo, shirika la utangazaji la CCTV limesema, tukio hilo "limehusisha watu 49, 19 kati yao walithibitishwa kufariki."
Maisha ya waliolazwa hospitalini hayako hatarini, CCTV imesema.
Picha zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii na kuripotiwa katika vyombo vya habari nchini humo zinaonyesha moshi na miali ya moto ikipanda kutoka kwenye shimo refu ambapo magari hayo yalitumbukia. Mamlaka imetangaza kutumwa kwa karibu watu 500 kusaidia juhudi za misaada, kulingana na vyombo vya habari vya serikali.
Sababu ya kuporomoka kwa barabara kuu hiyo bado haijatajwa.
Mkoa wa Guangdong umekumbwa na mfululizo wa matukio mabaya ya hali ya hewa katika wiki za hivi karibuni, kuanzia mafuriko mabaya hadi kimbunga kiharibifu.