Slovakia: Waziri Mkuu Robert Fico ajeruhiwa kwa risasi
Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico amejeruhiwa kwa risasi leo Jumatano baada ya kutoka kwenye mkutano wa serikali, shirika la habari la TASR linaripoti, likimnukuu Naibu spika wa Bunge, Lubos Blaha. Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, amelazwa hospitalini. Mshukiwa ameripotiwa kukamatwa.
Imechapishwa:
Kulingana na kituo cha habari cha Slovakia TA3, mshambuliaji alimpiga risasi nne kiongozi huyo anayeunga mkono Urusi na risasi moja tumboni. Mwandishi wa habari wa REUTERS katika eneo la tukio, nje ya mji mkuu Bratislava, alisikia milio kadhaa ya risasi na kuona polisi wakimkamata mshukiwa. Sababu ya shambulio hilo bado haijajulikana.
Rais wa Slovakia Zuzana Caputova amelaani shambulio la "kinyama" na kumtakia ahueni njema Robert Fico, ambaye alikua Waziri Mkuu tena mwaka jana baada ya kuwa tayari kushika wadhifa huu kati ya mwaka 2012 na 2018. Kiongozi huyo alijipambanua haswa kwa kukataa kuendelea kusaidia Ukraine kijeshi dhidi ya uvamizi wa Urusi.
WATCH: Slovakia's Prime Minister Fico taken to his car after shooting, current condition unknown pic.twitter.com/l7S2eaAEHp
— BNO News (@BNONews) May 15, 2024
(Taarifa zaidi zinakujia...)