Pata taarifa kuu

China: Maswali mengi tata kwenye ajenda ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anaanza ziara ya siku tatu nchini China leo Jumatano, Aprili 24, akiwa na orodha ndefu ya maswali ya kujadili na wenzake wake wa China, wakati uhusiano kati ya China na Marekani, ambao ulikuwa katika kiwango cha chini zaidi kwa mwakammoja uliyopita, unaendelea kuwa wa wasiwasi. Na China haina nia ya kutishwa, kulingana na taarifa zake rasmi za hivi punde.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, hapa ilikuwa mwezi wa Februari 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, hapa ilikuwa mwezi wa Februari 2024. © Mark Schiefelbein / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Florence de Changy

Katika tahariri iliyochapishwa Jumatano asubuhi na Xinhua, shirika la habari la serikali ya China, kabla tu ya kuwasili kwa Antony Blinken huko Shanghai, viongozi wamepongeza. Licha ya utulivu wa hivi majuzi wa uhusiano baina ya nchi hizo mbili, "uadui mkubwa unabaki" na hasa ni kosa la Marekani, tahariri inaonyesha.

Kuhusu suala gumu la mauzo ya nje ya China, Xinhua inaona hofu ya Washington kuwa isiyo na mantiki na inakemea matamshi ya Marekani yanayozidi kuwa pinzani.

China moja, msingi wa uhusiano wa China na Marekani

Swali la pili linalokasirisha: Taiwan na Bahari ya Kusini ya China. Tahariri hiyo inakumbusha kanuni ya China moja, msingi wa uhusiano wa China na Marekani. Na inashutumu kuingiliwa kwa Bahari ya Kusini ya China na Marekani ambayo "inasababisha mzozo kati ya China na majirani zake".

Hatimaye kuhusu suala la Ukraine, ambapo Marekani ingependa kuiona China ikichukua nafasi ya wazi zaidi na rais wa Ursi na sio kuchochea juhudi zake za vita, tahariri hiyo kinyume chake inaitaka Washington kutambua nafasi yake katika kuzidisha mgogoro huo na kuzidisha hali ya wasiwasi na kuacha kuilaumu China kila mara. Itoshe tu kusema kwamba nchi hizo zinamtazamo tofauti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.