Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Blinken awasili china kuweka shinikizo kwa Beijing kutunza amani na utulivu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili nchini China siku ya Jumatano kwa ziara yake ya pili katika muda wa chini ya mwaka mmoja, akiwa na ujumbe wa kuongeza shinikizo kwa Beijing katika masuala mbalimbali, kama vile uungaji mkono wake kwa Urusi, huku akitafuta utulivu mkubwa zaidi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akisalimiana na Kong Fuan, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Shanghai, Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Watu wa China R. Nicholas Burns na Balozi Mdogo wa Marekani Shanghai Scott Walker, alipowasili Shanghai, China tarehe 24 Aprili. 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akisalimiana na Kong Fuan, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Shanghai, Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Watu wa China R. Nicholas Burns na Balozi Mdogo wa Marekani Shanghai Scott Walker, alipowasili Shanghai, China tarehe 24 Aprili. 2024. via REUTERS - Mark Schiefelbein
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa diplomasia ya Marekani alitua Shanghai siku ya Jumatano, shirika la habari la AFP limebainisha, jiji ambalo anatarajiwa kukutana na wanafunzi na viongozi wa biashara.

Kituo hiki, kilichokusudiwa kuonyesha uhusiano mzuri kati ya Wamarekani na Wachina, ni cha kwanza mjini Shanghai kwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani tangu Hillary Clinton mwaka 2010.

Bwana Blinken atafanya mazungumzo na viongozi wa China mjini Beijing siku ya Ijumaa, ambapo anatarajiwa kuomba kujizuia huku Taiwan ikijiandaa kumuapisha rais mpya.

Ataelezea pia wasiwasi wa Marekani kuhusu biashara ya China, ambayo Washington inaona kuwa ni dhidi ya ushindani, suala muhimu kwa Rais Joe Biden katika mwaka huu wa uchaguzi.

Antony Blinken pia yuko nchini China ili kupunguza mvutano kati ya nchi hizo mbili zenye uchumi mkubwa duniani.

Haya yamepungua kwa kiasi kikubwa tangu ziara ya Bw. Blinken mwezi Juni.

Safari hii ilifuatiwa na mkutano kati ya Joe Biden na Rais wa China Xi Jinping mjini San Francisco mwezi Novemba, na kusababisha kuanzishwa tena kwa mawasiliano kati ya majeshi yao mawili na ushirikiano katika mapambano dhidi ya utengenezaji wa fentanyl, dawa ya syntetisk ambayo inaleta uharibifu mkubwa nchini. Marekani.

Waziri wa Fedha Janet Yellen pia alitembelea mji wa viwanda wa Guangzhou kabla ya kuelekea Beijing mapema mwezi huu.

Mahusiano ya China na Marekani yako katika "hatua tofauti na tulipokuwa mwaka mmoja uliopita, wakati uhusiano wa nchi mbili ulikuwa katika kiwango cha chini kihistoria," afisa mkuu wa Marekani alibainisha kabla ya ziara ya Antony Blinken.

"Pia tunaamini, na tumedhihirisha wazi kwamba usimamizi wa ushindani unaowajibika haimaanishi kwamba ni lazima tuache kuchukua hatua za kulinda maslahi ya kitaifa ya Marekani," alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.