Pata taarifa kuu

Watu 100,000 wa Korea Kaskazini wanafanya kazi ng'ambo kwa niaba ya utawala, ripoti inasema

Kulingana na matokeo ya ripoti ya kamati ya wataalamu ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mwezi huu, Wakorea Kaskazini 100,000 wanaendelea kufanya kazi nje ya nchi kwa ufadhili wa serikali ya nchi hiyo, licha ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Takwimu ambayo inaweza kuongezeka katika miaka ijayo.

Wafanyakazi huenda kufanya kazi katika kiwanda huko Dandong, mji wa China kwenye mpaka wa Korea Kaskazini. (Picha ya kielelezo)
Wafanyakazi huenda kufanya kazi katika kiwanda huko Dandong, mji wa China kwenye mpaka wa Korea Kaskazini. (Picha ya kielelezo) AP
Matangazo ya kibiashara

Licha ya mipaka iliyofungwa kwa muda mrefu na vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, bado kuna wastani wa Wakorea Kaskazini 100,000 wanaofanya kazi nje ya nchi. Ripoti ya kamati ya wataalamu kuhusu vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini inabainisha sekta ambazo wafanyakazi hawa, mara nyingi waathiriwa wa kutumiwa, hufanya kazi. Wanafanya kazi katika takriban nchi arobaini, wafanyakazi hawa wanafanya kazi katika teknolojia ya habari, ujenzi na afya.

Zoezi hili la kihistoria la utawala lilipaswa kumalizika mwezi wa Desemba 2019, tarehe ya mwisho ambayo nchi zote zililazimika kuwarejesha nyumbani wafanyakazi wa Korea Kaskazini, kulingana na Azimio 2,397 la Baraza la Usalama. Lakini wataalam wanahakikishia kwamba sio nchi zote zinzozingatia vikwazo.

Nusu ya dola bilioni ya mapato kwa Pyongyang

Nchi mbili haswa zinapokea idadi kubwa ya wafanyakazi kutoka Korea Kaskazini, kulingana na ripoti hiyo, ambayo haijataja majina ya nchi hizo. Uwepo wa wafanyakazi wa Korea Kaskazini nchini China, au wakataji miti na wafanyakazi wa ujenzi katika Mashariki ya Urusi, umeorodheshwa mara nyingi.

Wafanyakazi hawa wa kigeni wanawakilisha zaidi ya dola milioni 500 katika mapato ya kila mwaka kwa Pyongyang. Takwimu ambayo inaweza kuongezeka kwa kiasi kikubwa. Wataalamu wanahakikisha kwamba mara tu mipaka itapofunguliwa, serikali itapaswa kutuma wafanyakazi wengi nje ya nchi. Korea Kaskazini ilihitimisha makubaliano ya kuwatuma Wakorea Kaskazini 400,000 nje ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.