Pata taarifa kuu

Baraza la mpito la Haiti laahidi kurejesha utulivu wa umma

Mengi yanasubiriwa, baraza la mpito la Haiti, ambalo litachukuwa hatamu ya nchi baada ya tangazo la kujiuzulu kwa Waziri Mkuu aliyepingwa, liliahidi siku ya Jumatano katika taarifa yake ya kwanza kwa vyombo vya habari kurejesha "utulivu na kidemokrasia".

Maafisa wa polisi wakiwarushia vitoa machozi waandamanaji wakati wa maandamano, Port-au-Prince, Haiti, Agosti 14, 2023.
Maafisa wa polisi wakiwarushia vitoa machozi waandamanaji wakati wa maandamano, Port-au-Prince, Haiti, Agosti 14, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Mara tu litakapotangazwa, baraza la mpito litamteua Waziri Mkuu, ambaye naye ataunda serikali ya umoja wa kitaifa na kuirejesha Haiti kwenye njia ya uhalali wa kidemokrasia, utulivu na utu," wanaandika wajumbe wa chombo hiki ambacho bado hakijaanzishwa rasmi.

"Pamoja tutatekeleza mpango kazi wazi unaolenga kurejesha utulivu wa umma na kidemokrasia," waliongeza.

"Tumedhamiria kupunguza mateso ya raia wa Haiti, walionaswa kwa muda mrefu kati ya utawala mbaya, vurugu nyingi na kutozingatia mitazamo na mahitaji yao," waliongeza.

Waziri Mkuu Ariel Henry alitangaza kujiuzulu mnamo Machi 11, wakati Haiti, ambayo tayari iko katika mzozo mkubwa wa kisiasa na usalama, ilikuwa ikikumbwa na ghasia mpya.

Siku hiyo, wakati wa mkutano kati ya wawakilishi wa Haiti na wale wa nchi na mashirika kadhaa ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Karibea (Caricom), uundaji wa baadaye wa baraza la mpito la rais ulitangazwa.

Chombo hiki kitawakilisha wadau wakuu wa kisiasa wa Haiti pamoja na sekta ya kibinafsi, mashirika ya kiraia naviongozi wa kidini. Inaundwa na wapiga kura saba na waangalizi wawili ambao hawana haki ya kupiga kura.

Uzinduzi wa kundi hili ulicheleweshwa na mizozo ya ndani.

Taarifa kwa vyombo vya habari ya siu ya Jumatano, iliyotiwa saini na wajumbe wake wanane kati ya tisa, inaonekana kuwa hatua kuelekea kuanzishwa kwa mamlaka mpya. Ujio wa hivi punde zaidi wa wawakilishi wa baraza umeteuliwa.

Wajumbe hao walithibitisha katika maandishi yao kuwa wamekubaliana juu ya "vigezo na taratibu za uchaguzi wa rais au mwenyekiti wa baraza la rais", pamoja na uteuzi wa Waziri Mkuu wa mpito na baraza la mawaziri.

Wakati huo huo, idadi ya watu inaendelea kulipa bei kubwa kwa ukosefu wa utulivu.

Magenge yanadhibiti maeneo yote ya nchi, ikiwa ni pamoja na 80% ya mji mkuu wa Port-au-Prince.

Mkuu wa Unicef, Catherine Russell, alionya wiki hii kwamba "watoto wasiohesabika" wana hatari ya kupoteza maisha kutokana na mzozo wa pande nyingi unaoikumba Haiti, "wakati misaada muhimu iko tayari kusambazwa ikiwa ghasia zitasimama na barabara na hospitali kufunguliwa tena."

Kenya ilitakiwa kutuma maafisa elfu moja wa polisi nchini Haiti kama sehemu ya ujumbe unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, lakini ikatangaza kuwa inasimamisha mpango wake wa kutuma kikosi hicho kwa kuzingatia hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.