Pata taarifa kuu

Peru yashtumiwa kwa ukiukaji wa haki ya 'mazingira salama'

Ni hukumu ya kihistoria ambayo itakuwa mfano wa kuigwa katika bara zima la Amerika Kusini na kwingineko: Ijumaa Machi 22, 2024, Mahakama ya Haki za Kibinadamu ya Amerika (IACHR) ililaani Peru kwa kukiuka haki ya mazingira endelevu na yenye afya” ya wakazi wa mji wa madini katika Andes. Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kuwajibishwa kwa kushindwa kuwalinda raia wake dhidi ya uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na mashirika ya kimataifa.

Muonekano wa angani wa kampuni ya uchimbaji madini iliyoko katika mji wa La Oroya, Peru, Novemba 9, 2022.
Muonekano wa angani wa kampuni ya uchimbaji madini iliyoko katika mji wa La Oroya, Peru, Novemba 9, 2022. AFP - ERNESTO BENAVIDES
Matangazo ya kibiashara

La Oroya ni mojawapo ya miji kumi iliyoathiriwa zaidi duniani. Ni hapa, katika mwinuko wa mita 3,750 na kilomita 135 mashariki mwa Lima, ambapo kampuni ya uchimbaji madini inachimba madini ya shaba, zinki, risasi, fedha na dhahabu kutoka kwa migodi jirani kwa karne moja.

Kwa vizazi kadhaa, wakazi 20,000 wa La Oroya wamekabiliwa na uchafuzi wa metali nzito katika hewa, udongo na maji. Wanakabiliwa na kila aina ya magonjwa na utasa. Serikali ilijua hili, lakini haikuweka kanuni zozote kwa mashirika ya kimataifa - ikiwa ni pamoja na kampuni ya Marekani ya Renco - ambazo yalipishana kwenye eneo hili.

Mnamo mwaka 2006, waathiriwa 80 waliwasilisha malalamiko. IACHR imethibitisha tu kuwa wako sahihi. Majaji wameigiza serikali ya Peru, pamoja na mambo mengine, kuwashtaki waliohusika na uchafuzi wa mazingira, kutoa huduma ya matibabu ya bure kwa waathiriwa, kufidia uharibifu wote uliopatikana na kuandaa mpango wa usafi wa jiji.

Hukumu hii inajenga kielelezo muhimu: inaweka wajibu wa Serikali katika udhibiti wa makampuni na matokeo ya shughuli zao kwenye mazingira. Rosa Peña, mjumbe wa shirika la Kimataifa la Ulinzi wa Mazingira la Amerika na wakili wa waathiriwa wa La Oroya, anaelezea Raphaël Moran, wa RFI, changamoto kwa uamuzi huu mkuu:

“Hukumu hii inatambua wajibu wa Serikali katika ukiukaji wa haki za kuishi,  haki ya mazingira endelevu na yenye afya, kupata habari. Na inaweka hatua za fidia, kama vile jukumu la kutoa utambuzi juu ya usafi wa mazingira muhimu, hatua zilizowekwa maalum kwa waathiriwa na sio tu kwa walalamikaji, lakini kwa wakaazi wote wa La Oroya kwa ujumla, ili kwa mfano, watu wote ambao afya yao ilidhoofika na uchafuzi wa mazingira wanaweza kupata huduma ya bure. Uamuzi huo pia unasema kwamba Serikali lazima iombe hadharani msamaha kutoka kwa watu na lazima iwafidie kifedha waathiriwa kwa uharibifu uliopatikana. Hii ni hukumu ya kwanza iliyotolewa na Mahakama ya Haki za Kibinadamu ya Amerika (IACHR) inayotambua haki ya mazingira yenye afya. Kwa hivyo hii ni hatua endelevu kwa Mahakama ya Haki za Kibinadamu ya Amerika ya Kusini, mfano ambao unaweza kutumika kwa kesi zingine katika eneo hilo. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.