Pata taarifa kuu

Makubaliano ya nafaka: Erdogan aahidi tangazo 'muhimu', Putin 'yuko tayari' kwa majadiliano

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameahidi atakapowasili Sochi (Urusi) Jumatatu hii atatoa tangazo "muhimu sana" kuhusu usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine kufuatia mkutano wake na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin. Rais wa Urusi ameitangaza kuwa "yuko tayari kwa majadiliano".

Rais wa Urusi Vladimir Putin amempokea mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan huko Sochi mnamo Jumatatu Septemba 4, 2023: katika ajenda ya mazungumzo, kinachojulikana kama makubaliano ya nafaka ya Bahari Nyeusi ambayo Urusi ilijiondoa.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amempokea mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan huko Sochi mnamo Jumatatu Septemba 4, 2023: katika ajenda ya mazungumzo, kinachojulikana kama makubaliano ya nafaka ya Bahari Nyeusi ambayo Urusi ilijiondoa. AFP - MIKHAIL KLIMENTYEV
Matangazo ya kibiashara

"Ninaamini kwamba ujumbe ambao tutawasilisha katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano wetu utakuwa muhimu sana kwa ulimwengu, hasa kwa nchi za Afrika zinazoendelea," rais wa Uturuki amesema.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema yuko "tayari kwa majadiliano" siku ya Jumatatu na Bw. Erdogan juu ya makubaliano ya kuruhusu usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine kupitia Bahari Nyeusi, ambayo Moscow ilijondoa Julai 17 na kwamba tangu wakati huo 'Ankara imekuwa ikijaribu kufufua. Urusi inasema kuwa kupeleka bidhaa zake za kilimo na mbolea kwenye soko la kimataifa kunatatizwa na vikwazo vya Magharibi.

Mkuu wa serikali ya Uturuki, akifambatana mjini Sochi na mawaziri wake wa Mambo ya Nje, Ulinzi, Fedha na Nishati, anatumai kufanya majadiliano haya kuhusu usafirishaji wa nafaka ya Ukraine kuwa chachu ya mazungumzo ya amani kati ya Kiev na Moscow.

Recep Tayyip Erdogan anajua kwamba wakati si mzuri wa kuzindua upya suala hili. Wanajeshi wa Urusi wanaokabiliana na mashambulizi ya Kiev ambayo yanaonekana kushika kasi katika siku za hivi karibuni, huku Moscow ikiongeza mashambulizi dhidi ya miundombinu ya bandari ya Ukraine ambayo meli zinazohusika na usafirishaji wa nafaka hupitia. Lakini rais wa Uturuki ana uhakika kuwa hakuna njia mbadala ya makubaliano haya, amekumbusha mwandishi wetu huko Istanbul, Anne Andlauer Kwa kifupi: lazima tufikie makubaliano na Moscow ili usafirishaji wa nafaka za Ukraine kupitia bahari Nyeusi uanze tena kwa usalama na njia ya gharama nafuu iwezekanavyo.

Rais wa Uturuki anategemea uhusiano wake wa kipekee na Vladimir Putin, licha ya mivutano kadhaa katika miezi ya hivi karibuni, kutafuta mwafaka ili kurejesha makubaliano ya usafirishaji wa nafaka.

Mkataba muhimu ili kuepuka mzozo wa chakula duniani. Moscow imekuwa ikirudia kwa miezi kadhaa kwamba nchi za Magharibi lazima ziheshimu ahadi zao kwa Urusi kuzindua tena makubaliano haya, ambayo Recep Tayyip Erdogan alisisitiza mwanzoni mwa mwezi Agosti.

Madai ambayo ni sawa na kuondolewa kwa sehemu ya vikwazo vilivyowekwa mwanzoni mwa mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine. Maombi ambayo nchi washirika wa Kyiv hazionekani kulichukuliwa sawa, isipokuwa Recep Tayyip Erdogan aweze kutoa ushawishi katika mkutano wa kilele wa G20 ambao utafanyika chini ya wiki moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.