Pata taarifa kuu

Upinzani nchini Kenya kurejelea maandamano siku ya Jumanne

Nairobi – Upinzani nchini Kenya, unaongozwa na Raila Odinga, utarejelea  siku ya Jumanne, maandamano ya kupinga kupanda gharama ya maisha na kufanyika mageuzi muhimu ya uchaguzi licha ya serikali kuapa kuwazuia waandamanaji hao kwa madai kuwa wanalenga kuharibu amani ya nchi.

Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, pamoja na rais William Ruto
Raila Odinga kiongozi wa upinzani nchini Kenya, pamoja na rais William Ruto © AFP
Matangazo ya kibiashara

Odinga  amesema maandamano hayo yatakuwa ya amani na yataanza saa 12 Alfajiri jijini Nairobi, na waandamanaji watakwenda katika ofisi ya rais na ofisi ya Tume ya Uchaguzi.

Hapatakuwa na uharibifu wa mali ,hicho ni kisingizio tu,watu wetu wameshauriwa kuwa watulivu,tumesema tutaandamana kwenye bustani la Central, kisha tutafululiza mpaka ofisi za IEBC ambapo tutawasilisha ombi letu
00:20

Raila Odinga, Kiongozi wa upinzani nchini Kenya

Awali akiongoza wakenya kuadhimisha sherehe hizo wa leba ,rais William Ruto alisema serikali itanya iwezavyo kuzuia uharibifu wa mali na kuathirika shughuli za kiuchumi wakati wa maandamano.

Hata ubebe sufuria kwa kicha siku ngapi, bei ya unga itarudi chini ? Sita ruhusu mali ya mwananchi kuharibiwa, kazi ya mwananchin kuharibika, biashara ya mwananchi kuharabika, kazi ya mwananchi kuharibika, watoto wasiende shule kwasababu kuna watu wanataka tugawane serikali. Hiyo haitafanyika. Hiyo ingine watafute kule bungeni
00:36

William Ruto, Rais wa Kenya

Viongozi hao wawili siku za hapo nyuma walikubaliana kusitishwa kwa maandamano na kufanyika mazungumzo ya mapatano kupitia bunge ,mazungumzo ambayo yameendelea kusuasua.

Maandamano haya yanaenda kufanyika huku kamati za wabunge kutoka pande zinazozozana, wakiendelea kuvutana, kitendo kinachodhihirisha kuwa huenda kusipatikane muafaka licha ya mwito wa rais Ruto na Odinga mwenyewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.