Pata taarifa kuu

Nishati: Nchi za magharibi kupunguza bei ya bidhaa za petroli za Urusi

Kufuatia makubaliano ya Umoja wa Ulaya, G7 na Australia zimekubali kupunguza bei ya bidhaa za petroli za Urusi. Utaratibu huo unatarajiwa kuanza kutumika Jumapili hii, Februari 5, wakati mmoja na marufuku ya Ulaya au "muda mfupi baadaye". Lengo lililotajwa: "Kuzuia Urusi kunufaika" kutokana na kuongezeka kwa bei zinazohusishwa na vita vya Ukraine na "kuunga mkono utulivu" wa soko. Mkataba huu unasema nini?

Meli za mafuta katika bandari ya Nakhodka (Urusi), mnamo Desemba 4, 2022.
Meli za mafuta katika bandari ya Nakhodka (Urusi), mnamo Desemba 4, 2022. © Reuters/Tatiana Meel
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo unalingana na mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Ulaya. Kwa bidhaa za gharama kubwa zaidi, kama vile dizeli, bei ya juu kwa pipa imewekwa kwa dola 100. Kwa bidhaa zilizosafishwa kidogo kama , pipa moja imewekwa kwa euro 45.

Boti kutoka nchi washirika

Hii inahusu bidhaa zinazosafirishwa na meli kutoka nchi washirika. Zaidi ya kiasi hiki, makampuni yaliyo katika Umoja wa Ulaya, G7 na Australia yatapigwa marufuku kutoa huduma zinazoruhusu usafirishaji, ikiwa ni pamoja na bima. Hata hivyo, nchi za G7 hushughulikia takriban 90% ya shehena ya kimataifa.

Poland na Mataifa ya Baltic yalikuwa yakidai, kulingana na vyanzo vya kidiplomasia, bei ya chini ili kuadhibu zaidi Moscow. Lakini hesabu zimechanganya. Nchi zenye nguvu za G7 na Australia zinanuia kuipiga Moscow kwenye mfuko wa fedha bila kuizuia Urusi kuendelea kutoa bidaa zake katika soko la dunia. Hii inaweza kuwa na athari ya kudhoofisha biashara na inaweza kusababisha bei kupanda.

Masoko yasiyo na usawa?

Moscow pia inawasiliana juu ya suala hili. Urusi inahakikisha kwamba vikwazo vya Ulaya vitazidisha usawa katika masoko ya kimataifa ya nishati na kusema kuwa inachukua hatua kufidia maslahi yake.

Utaratibu ambao utaanza kutumika Jumapili hii ni sawa na ule ambao tayari umetekelezwa kwa mafuta ghafi mwanzoni mwa mwezi Desemba. Ni vigumu kutabiri athari halisi ya vikwazo hivi vipya. Lakini Samuel Furfari, profesa wa siasa za jiografia ya nishati katika Chuo Kikuu Huria cha Brussels, anabainisha kuwa juu ya mafuta ghafi, mifumo hii haijasababisha mapinduzi.

"Mahitaji hayana nguvu. Tunaweza kuweka vikwazo, lakini watu wanahitaji kuzunguka ulimwenguni, anaelezea mtafiti. Kilichotokea hapa inaonekana ni kwamba mafuta hayajapata pigo, kwa sababu kwanza soko daima lina hitaji mengi. Na juu ya yote, kilichotokea ni kwamba hatukuuza mafuta ya Urusi kwa Umoja wa Ulaya, lakini India, China na nchi nyingine walinunua. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.