Pata taarifa kuu

Kenya:Hali ya kawaida yarejea baada ya Ruto na Raila kukubali kufanya mazungumzo

Nairobi – Shughuli za kawaida zimeonekana kuendelea jijini Nairobi nchini Kenya baada ya hapo jana kinara wa Upinzani Raila Odinga kusitisha maandamano.Hii inakuja baada ya pande hizo mbili kukubaliana kufanya mazungumzo.

Rais wa Kenya William Ruto wakubaliana  kufanya mazungumzo na kinara wa upinzani Raila Odinga
Rais wa Kenya William Ruto wakubaliana kufanya mazungumzo na kinara wa upinzani Raila Odinga AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Hali imereja kama kawaida jijini Nairobi huku kila mmoja na pilka pilka zake. Raia wakifurahishwa sana na hatua ya kinara wa Azimio ya kutupilia mbali maandamano.

“Naitwa Joseph  Wabwire hatukutarajia na ilishtua watu ,kuna wengine hawajafurahia na wengine wanatamani serikali ingendelea kusukumwa ili hali ya maisha irudi chini.”amesema raia wa Kenya,Joseph  Wabwire.
00:14

Wabwire kuhusu,hutukutarajia kauli hiyo

 Hali kama hii  pia ilishuhudiwa katika kaunti mbalimbali ambazo zimekuwa zikiandaa maandamano. Biashara na masomo ambayo yalitatizika wiki mbili zilizopita, safari hii zikireja kama kawaida. Wananchi nao wakijifunza mawili matatu kutokana na maandamano.

“Na mwisho mwisho mtakuja kuona ,wakati watashikana mtakuja kuona ,hiyo unga tutanunua hata mia 500.ameelezea Raia mmoja Wakenya kwenye mitaa ya jiji kuu
00:16

Raia mmoja wa Kenya ,Nairobi

Kinacho subiriwa sasa ni kuona ikiwa nafasi ya mazungumzo kati ya upinzani na Serikali itazaa matunda katika siku sita zijazo.

Muungano wa Afrika Mashariki, Igad, ,pia umempongeza Rais wa Kenya William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa kukubali kufanya mazungumzo yenye lengo la kumaliza wiki mbili za maandamano kuhusu gharama ya maisha na mageuzi katika mfumo wa uchaguzi.

Maandamano ya wiki mbili sasa katika taifa hilo la Afrika Mashariki, yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali, mamia ya raia wakiripotiwa kujeruhiwa wakiwemo maofisa ya polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.