Pata taarifa kuu
CHAD-SIASA

Wafuasi kadhaa wa upinzani nchini Chad waachiwa

Nchini Chad, wafuasi kadhaa wa upinzani waliokamatwa katikati mwa mwezi Novemba waliachiliwa Jumatano wiki hii na mahakama. wafuasi hao walikamatwa wakijaribu kufanya maandamnao baada ya kupigwa marufuku kufanya mkutano uliokua ulipangwa kufanyika Novemba 17.

Soldats tchadiens devant le tribunal de Ndjamena (image d’archive 2007).
Soldats tchadiens devant le tribunal de Ndjamena (image d’archive 2007). Thomas SAMSON/Gamma-Rapho via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi hao wa upinzani waliachiwa baada ya mahakama kuona kuwa waliku hawana hatia. Kabla ya mahakama kutoa uamuzi wake, Mwendesha mashitaka alisikika akisema mbele ya majaji kwamba "Hatupaswi kuingilia vyombo vya sheria katika masuala ya kisiasa".

Wafuasi hao wa upinzani walioshtumiwa kukusanyika bila silaha waliachiwa kwa kosa ambalo halikuzingatiwa na mahakama, huku wanasheria wao wakionyesha furaha kubwa waliokuwa nayo "Walikutana kwa mazungumzo. Na wakati walipokua wakirejea makwao polisi iliwakamata wakiwa katika magari. Polisi ilivunja madirisha ya magari, na kitendo hiki kiovu, tunaomba kisirudii tena. Demokrasia nchini Chad inakwenda vizuri. Na hakuna kitu kitakachoizuia. Kila mtu anapaswa kuelewa, " mmoja wa wanasheria wa wafuasi wa upinzani amesema.

Upinzani kwa upande wake umekumbusha kuwa masuala mengine ya kisiasa bado yanajiri nchini Chad, ikiwa ni pamoja na Dinamou Daram, mkuu wa chama cha upinzani, ambaye bado anazuliwa. Anashtumiwa kuandika tangazo lililowataka kutolipa kodi. Anapaswa pia kuachiwa huru,upinzani umedai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.