Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-UCHUMI

Viongozi wa Sudan Kusini watupilia mbali ripoti ya The Sentry

Mahasimu wa vita vya wenyewe tangu miaka mitatu iliyopita nchini Sudan Kusini wamejitajirisha kupitia machafuko ya kivita yanayoendelea, muigizaji nyota wa Hollywood, George Clooney, ameshtumu Jumatatu wiki hii katika ripoti iliyotolewa mjini Washington.

Raais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kushoto) na mpinzani wake Riek Machar (kulia) wanashtumiwa kujitajirisha kupitia vita.
Raais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kushoto) na mpinzani wake Riek Machar (kulia) wanashtumiwa kujitajirisha kupitia vita.
Matangazo ya kibiashara

Muigizaji huyo kutoka Marekani ni mwanzilishi wa Shirika la Sentry linaloendesha uchunguzikuhusu ufadhili wa mgogoro barani .

Kwa upande wa viongozi wa Sudan Kusini, nchi iliyoanzishwa mwezi Julai mwaka 2011 chini ya udhamini wa Marekani, nchi ambayo inaendelea kukumbwa na vita vya wenyewe kwa tangu Desemba 2013, wamesema Bw Clooney aliwasilisha kazi yake kwa vyombo vya habari sambamba na muigizaji kutoka Marekani Don Cheadle na mwanaharakati wa haki za binadamu John Prendergast.

Waziri wa habari Sudan Kusini amesema kuwa serikali haijawa tayari kujibu madai ya ripoti hiyo inayodai kuwa viongozi wa Sudan Kusini wananufaika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinayoendelea nchini humo.

Michael Maquei Lueth amesema kuwa serikali ina mambo mengi ya kusema kuhusu madai hayo lakini iko tayari kutoa msimamo wake ikiwa itapatiwa rasmi taarifa za kina.

Nyota wa Marekani, anayejulikana harakati zake za kisiasa na kibinadamu, alipokelewa pia kwa muda "mfupi" na Rais Barack Obama, kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa Marekani.

Ripoti hiyo ya The Sentry inawatuhumu viongozi wa kisiasa na kijeshi nchini Sudan Kusini, Rais Salva Kiir akichukua nafasi ya kwanza na makamu wake wa zamani, Riek Machar, kwa kujitajirisha wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.