Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ANC

Uchaguzi hatari kwa ANC

Watu milioni 26 nchini Afrika Kusini wanatazamiwa kupiga kura Jumatano hii Agosti 3 kwa kuwachagua mameya wao na madiwani. Uchaguzi huu ambao ni kama mtihani kwa chama cha ANC, ambachoo kimekua kikionekana dhaifu katika utafiti uliyoendeshwa hivi karibuni.

Wafuasi wa chama tawala cha ANC, katika mitaa ya Vuwani, siku moja kabla ya uchaguzi wa majimbo.
Wafuasi wa chama tawala cha ANC, katika mitaa ya Vuwani, siku moja kabla ya uchaguzi wa majimbo. MUJAHID SAFODIEN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kashfa ya mara kwa mara na mdororo wa uchumi nchini humo ni sababu ya chama cha ANC kupoteza imani kwa wananchi. Cham hiki chenye wafuasi wengi pia nikimedhoofika na mgawanyiko wa ndani kati ya wafuasi na wapinzani wa Jacob Zuma.

Kwa matatizo haya kumeshuhudiwa kupungua kwa idadi ya wapiga kura wa jadi wa chama hiki tawala. Miaka ishirini na miwili baada ya kuanguka kwa utawala wa ubaguzi wa rangi na ujio wa demokrasia, raia wengi wa Afrika Kusini wanakishtumu chama cha ANC kutokufanya kazi ya kutosha.

Katika baadhi ya vitongoji, raia wengi wameathirika zaidi na ukosefu wa ajira na bado wanakabiliwa na ukosegu wa maji na umeme. Aidha, rushwa imekithiri hasa nchini humo katika ngazi ya mikoa, ambapo washauri wamekua wakitumia nyadhifa zao kwa kuwanufaisha ndugu zao.

Vyama vya upinzani kuwa makini

Mambo yote haya yanaweza kuhamasisha wapiga kura kwa zoezi hili la uchaguzi kwa kupinga chama cha hayati Nelson Madiba Mandela, mwasisi wa chama cha ANC. Na upinzani unatarajia kuchukua nafasi hii katika miji kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.