Pata taarifa kuu
MAREKANI-HILLARY CLINTON

Hillary Clinton ateuliwa rasmi kuwa mgombea wa Ikulu

Zaidi ya wajumbe 4,700 wa chama cha Democratic walikutana Jumanne hii Julai 26 katika mji wa Philadelphia, katika makubaliano ya kumpitisha mgombea wao katika uchaguzi wa urais. Wakati wa kikao hicho cha siku ya pili, Hillary Clinton aliteuliwa rasmi kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais.

Hillary Clinton, Julai 18, 2016 katika jimbo la Ohio.
Hillary Clinton, Julai 18, 2016 katika jimbo la Ohio. REUTERS/William Philpott
Matangazo ya kibiashara

Hillary Clinton, mwenye umri wa miaka 68, ambaye aliwahi kuhudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje anakuwa mwanamke wa kwanza akiikaribia Ikulu ya Marekani kama mgombea urais.

Hillary Clinton, mkee wa rais wa zamani wa Marekani, seneta wa zamani wa jimbo la New York na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, hatimaye ni mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais wa Marekani uliyopangwa kufanyika mwezi Novemba 2016. Zoezi la upigaji kura lilifanyika katika mazingira mazuri bila upinzani wowote. Hillary Clinton atabaki kuwa mwanamke wa kwanza kugombea katika chama ckikuu katika kinyanganyiro cha urais katika Ikulu ya White House, baada ya kushindwa kwake katika kura za mchujo mwaka 2008 dhidi ya Barack Obama, rais wa kwanza mweusi wa Marekani. Alichukua miaka kumi ya kufika kwenye hatua hii.

Jana Jumanne Bernie Sanders alionekana kuwaunganisha wafuasi wa chama hicho na kuwaomba kumuunga mkono Bi.Clinton na kuhakikisha kuwa anakuwa rais wa Marekani ifikapo mwezi Novemba.

Kabla ya kuanza kuzungumza, Seneta huyo wa jimbo la Vermont alishangiliwa kwa muda wa dakika tatu akiwa jukwani.

“Hillary Clinton ni lazima awe rais ajaye wa Marekani,” alisema huku akishangiliwa na maelfu ya wajumbe hao.

Mke wa rais Obama, Mitchel Obama naye alihotubia wajumbe hao na kukashifu matamshi ya mgombea wa upinzani Donald Trump na kuongeza kuwa Bi.Clinton ndio mwanasiasa pekee wa kuaminiwa kuiongoza Marekani.

“Mtu asiwadangaye kuwa taifa hili sio kuu, eti kwamba kuna mtu anataka kulifanya kuwa kuu tena,” alisema huku akishangiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.