Pata taarifa kuu
DRC-UPINZANI-MAANDAMANO

Makabiliano kati ya waandamanji na polisi yatokea Lubumbashi

Polisi mjini Lubumbashi Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamepambana na maelfu ya waandamanaji wa upinzani wanaomtaka rais Joseph Kabila kutowania tena urais mwezi Novemba mwaka huu.

Polisi ya kutuliza ghasia ya DRC ikitoa ulinzikenye barabara inayoelekea makao makuu ya chama cha UDPSmjini Lubumbashi tarehe 5 Desemba 2011.
Polisi ya kutuliza ghasia ya DRC ikitoa ulinzikenye barabara inayoelekea makao makuu ya chama cha UDPSmjini Lubumbashi tarehe 5 Desemba 2011. AFP / PHIL MOORE
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji hao walionekana wenye hasira huku wakitamka, Kabila lazima aondoke, aje atue, tumechoka, walisikika wakisema mbele ya Ofisi ya chama cha UNAFEC kinachoongozwa naAntoine-Gabriel Kyungu wa Kumwanza.

Kumekuwa na madai kuwa rais Kabila ambaye muhula wake unakamilika mwezi Novemba anapanga kubadilisha Katiba ili awanie tena urais kwa muhula wa watatu.

Wakati huo huo jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FARDC linasema linaendelea na msako kuwatafuta waasi waliowateka nyara wafanyakazi watano wa Shirika la Kimataifa la misaada ya kibinadamu Mercy Corps waliokuwa katika eneo la Nyanzale wakiwa njiani kwenda Bwalanda Mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.