Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Wimbi la siasa: Madai ya Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu nchini Burundi
Kwenye Makala haya Ali Bilali akiwa pamoja na wachambuzi wa siasa Mali Ali kutoka Paris Ufaransa na Abdulkarim Atiki wanaangazi kuhusu tuhuma za Burundi kwa Rwanda kuhusika na vitendo vya uhalifu hususan uvurumishaji guruneti katika mji wa Bujumbura, tukio la hivi karibuni liligharimu maisha ya watu kadhaa na kuwajeruhi wengine.17/05/202410:01 -
Serikali ya Sudan Kusini na makundi ya waasi yaanza mazungumzo jijini Nairobi
Mazungumzo ya amani yanayohusisha makundi ya waasi nchini Sudan Kusini na serikali yameanza rasmi jijini Nairobi, wakati huu taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi wa mwezi Disemba.10/05/202410:05 -
Nini haki za wafanyakazi duniani ?
Kila tarehe 1, ni maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi duniani. Wafanyakazi wanatumia siku hii kusherehekea mafanikio yao na kuendeleza mapambano ya haki zao. Je, siku hii ina umuhimu gani ? Wageni wetu ni Nice Mwansasu kutoka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na mwanasheria wa masuala ya ajira kutoka Kenya Elvis Abenga01/05/202410:13 -
Mwaka mmoja wa mapigano nchini Sudan kati ya jeshi la serikali na RSF
Wiki hii, ilikuwa ni mwaka mmoja wa vita nchini Sudan, kati ya jeshi la taifa chini ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wa RSF wanaongozwa na Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo.17/04/202409:34 -
Uhusiano kati ya Somalia na Ethiopia waendelea kuingia baridi
Wiki iliyopita, Somalia ilimfukuza nchini mwake Balozi wa Ethiopia Mukhtar Mohamed kwa madai kuwa nchi hiyo inaingilia mambo yake ya ndani.Mwezi Januari, mzozo wa kidiplomasia ulianza kushuhudiwa nchini humo baada ya Ethiopia kuingia kwenye makubaliano na jimbo la Somaliland, kutafuta njia ya kufika baharini na kujenga kambi ya jeshi kwenye ukanda wake wa pwani.Nini hatima ya mvutano huu ?10/04/202409:21 -
Maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ,ulimwengu umejifunza nini?
Kumbikizi ya miaka 30 tangu mauaji ya kimbari yaliyosababisha vifo vya watu hadi laki 8 ,kuna wito wa ulimwengu kuhakikisha watuhumiwa zaidi kusakwa na mataifa yaweke mikakati kuzuia mauaji kama haya kutojirudia03/04/202409:48 -
Raia wa Senegal wamchagua Faye kuwa rais wao mpya
Bassirou Diomaye Faye amechaguliwa kuwa rais mpya wa Senegal.Faye mwenye umri wa miaka 44, mshirika wa karibu wa mwanasiasa mwenye ushawishi Ousamane Sonko, ameahidi kufungua ukura mpya wa uongozi wa nchi hiyo.Kwanini raia wa Senegal wamemchagua Faye ? Tunachambua pamoja na Mali Ali akiwa jijini Paris, na Lutege Musa Lutege akiwa jijini Dar es salaam.27/03/202410:15 -
Makala haya yanatupia jicho uchaguzi wa urais nchini Urusi, nini maana ya ushindi wa rais Vladimir Putin.
20/03/202410:04 -
Burundi: Mgawanyiko kwenye chama kikuu cha upinzani CNL
Nchini Burundi, chama kikuu cha upinzani cha CNL kinashuhudia mgawanyiko baada ya kiongozi wake Agathon Rwasa kuondolewa kwenye nafasi kiongozi wa chama.Hii ilitokea wakati Rwasa akiwa ziarani nchini Kenya.Nini hatima ya kisiasa ya Rwasa ?Tunazungumza naye lakini pia Mali Ali mchambuzi wa siasa za Burundi akiwa jijini Paris.13/03/202410:22 -
Kenya: Kutuma polisi wake nchini Haiti kuthibiti magenge ya wahalifu
Serikali ya Kenya na Haiti zimetiliana saini ili kufanikisha Kenya kutuma polisi wake nchini Haiti kudhibiti magenge ya wahalifu ambayo yameendelea kutatiza usalama nchini Haiti.08/03/202409:59 -
Uongozi wa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir katika jumuiya ya Afrika Mashariki
Rais Salva Kiir amekuwa ziarani Rwanda na Burundi kuangazia swala la usalama28/02/202410:14 -
AU yakosa kupata suluhu kwa mizozo ya Africa
Viongozi wa Africa wamekutana mwisho wa juma katika mkutano wao wa kila mwaka wa 37, nchini Ethiopia walishindwa kuja na njia ya mapoja kumaliza migogoro barani.21/02/202410:02 -
Wabunge nchini Tanzania wapitisha mageuzi ya sheria za uchaguzi
Wiki iliyopita, wabunge nchini Tanzania, walipitisha miswada mitatu ya sheria ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao. Tume ya uchaguzi itabadilishwa jina na sasa itafahamika kama Tume huru ya taifa ya Uchaguzi. Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake, watateuliwa na rais baada ya kupokea majina matatu kutoka kwenye Kamati ya usaili.Chama kikuu cha upinzani, CHADEMA kinapinga mabadiliko hayo.07/02/202409:40 -
Niger, Mali na Burkina Faso kujiondoa ndani ya ECOWAS
Mataifa ya Mali, Niger na Burkina Faso, yametangaza kujiondoa kwenye muungano wa ECOWAS, baada ya vikwazo ambayo muungano huu ulitangaza dhidi ya mataifa hayo, kipindi baada ya mapinduzi ya kijeshi.03/02/202409:42 -
Matarajio ya wakongo baada ya kuapishwa kwa rais Félix Tshisekedi
Wimbi la siasa imeangazia fursa iliyopo kidiplomasia kwa rais wa DRC Felix Thisekedi aliyeapishwa Jumamosi iliyopita, kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili.DR Congo, imekuwa kwenye mvutano wa kidiplomasia na Rwanda, kwa madai kuwa Kigali inawaunga mkono waasi wa M23 eneo la mashariki. Ruben Lukumbuka amewaalika Francois Alwende, mtaalamu wa siasa za DRC akiwa jijini Nairobi pia Guerschome Kahebe pia ni mchambuzi wa siasa akiwa Jijini Washington nchini Marekani.24/01/202410:11
Wimbi la Siasa
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa