Pata taarifa kuu

Kenya: Watu 118 waliuawa na polisi mwaka uliopita: Mashirika ya kiraia

Ripoti ya mashirika ya kutetea haki za binadamu ya ndani na nje ya nchi ya Kenya, imesema raia 118 walikuwa waathiriwa wa mauaji yanayotekelezwa na maofisa wa polisi mwaka jana.

Polisi wakupambana na ghasia katika mji wa Kibera jijini Nairobi, Kenya  Julai 19, 2023
Polisi wakupambana na ghasia katika mji wa Kibera jijini Nairobi, Kenya Julai 19, 2023 © Brian Inganga / AP
Matangazo ya kibiashara

Yakitoa ripoti hiyo, mashirika hayo yamelaani ukiukaji wa haki za binadamu unaotekelezwa na idara za usalama.

Mwaka wa 2022, watu 130 waliripotiwa kuuawa na polisi ikiwa ni asilimia 9 chini ya idadi ya wale waliouawa mwaka jana.

Aidha ripoti hiyo pia imeeleza kuwa idadi ya watu waliripotiwa kutoeka mikononi mwa polisi ilipungua kwa asilimia 10 katika kipindi hicho.

Maandamano yalioongozwa na upinzani kupinga kupanda kwa gharama ya maisha yalishuhudiwa mapema mwaka jana.
Maandamano yalioongozwa na upinzani kupinga kupanda kwa gharama ya maisha yalishuhudiwa mapema mwaka jana. AP - Brian Inganga

Karibia nusu ya mauaji hayo yalitekelezwa wakati wa oparesheni ya kupambana na uhalifu kwa mujibu wa Human Rights Watch, Amnesty International Kenya na shirika Kenyan group Missing Voices.

Joseph Kariuki ni kutoka shirika la kutetea haki za binadamu la International Justice Mission.

“Zile kesi ambazo tumepata haki zinaweza kuwa karibia 500, kesi ambazo raia wameshikwa na polisi kinyume na sheria na kisha polisi wanawashitaki kwa makosa ambayo hawakufanya.” aliesema Joseph Kariuki ni kutoka shirika la kutetea haki za binadamu la International Justice Mission.

00:33

Joseph Kariuki ni kutoka shirika la kutetea haki za binadamu la International Justice Mission

Watu wengine 45 waliuawa wakati wa maandamano ya upinzani kati ya mwezi Machin na Julai mwaka uliopita kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha kwa mujibu wa mashirika hayo.

Maandamano hayo dhidi ya serikali ya rais William Ruto yalishuhudia machafuko na kuporwa kwa mali, upinzani na mashirika ya kiraia yakiwatuhumu polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasia kuwakabili waandamanaji.

Wakati wa kuchapishwa kwa habari hii, msemaji wa polisi Resila Onyango hakuwa amezungumzia ripoti hii.

Polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani wakati wa maandamano yaliofanyika jijini Nairobi kupinga kupanda kwa gharama ya maisha awali
Polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani wakati wa maandamano yaliofanyika jijini Nairobi kupinga kupanda kwa gharama ya maisha awali REUTERS - JOHN MUCHUCHA

Tangu ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022, Rais Ruto ameendelea kusisitiza kuwa anataka kumaliza visa vya polisi kuwatowesha watu na kutekeleza mauaji kinyume na sheria.

Polisi nchini Kenya wamekuwa wakituhumiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu kwa kutumia nguvu kipita kiasi na kutekeleza mauaji kinyume na sheria haswa katika mitaa inayokaliwa na maskini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.