Pata taarifa kuu

Rais Ruto awaagiza wanajeshi kuwaokowa waliokumbwa na mafuriko

Rais wa Kenya Wiliam Ruto, ametuma jeshi kusaidia kuwaondoa watu waliokwama kwenye maeneo yanayoshuhudia mafuriko makubwa kufuatia mvua inayoendelea kunyesha ambayo imesababisha vif vya watu zaidia ya 170 tangu mwezi Machi.

Wakaazi wa Nairobi wakijaribu kukusanya mali zao kufuatia mafuriko nchini Kenya.
Wakaazi wa Nairobi wakijaribu kukusanya mali zao kufuatia mafuriko nchini Kenya. © Monicah Mwangi / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Aidha, Ruto amewataka watu wanaoishi kwenye maeneo yenye hatari ya kukumbwa na mafuriko kuhama haraka iwezekanavyo.

Rais Ruto, ambaye aliwatembelea waathirika wa mkasa huo baada ya kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Nairobi, alisema serikali imechora ramani ya vijiji ambavyo vipo hatarini kukumbwa na mafuriko, wakati tahadhari ya mvua zaidi ikitolewa.

Zaidi ya watu 190,000 wameyakimbia makaazi yao wakiwemo 147,000 katika mji mkuu wa Nairobi, huku Idara ya Hali ya Hewa nchini himo ikisema bado maeneo kadhaa yalikuwa yakitarajiwa kupata mvua kubwa katika siku zijazo.

Wiki hii bwawa lilivunja kingo zake katika kijiji cha Kamuchiri, katika Kaunti ya Nakuru na kusababisha vifo vya karibu watu 50.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.