Pata taarifa kuu

Rais wa Uganda Yoweri Museveni yuko nchini Kenya kwa ziara ya kikazi

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewasili hapo jana jijini Nairobi nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni yuko nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni yuko nchini Kenya kwa ziara ya siku tatu. REUTERS - ABUBAKER LUBOWA
Matangazo ya kibiashara

Museveni anatarajiwa kushiriki mazungumzo na mwenyeji wake rais wa Kenya William Ruto hii leo alhamisi.

Rais Museveni alipokelewa na waziri wa mambo ya kigeni na mkuu wa mawaziri nchini Kenya, Musalia Mudavadi.

Ziara hiyo inafuatia kikao cha pili cha Tume ya Pamoja ya Mawaziri (JMC) kilichomalizika hivi karibuni kati ya Kenya na Uganda, ambapo mikataba saba ya makubaliano (MoU) ilisainiwa katika masuala mbalimbali ikiwemo utumishi wa umma, elimu, maendeleo ya biashara ndogo ndogo, michezo, masuala ya vijana,biashara na uwekezaji.

Kwa upande wake, waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Musalia Mudavadi, amesema kwamba ziara ya rais Museveni ni muhimu zaidi na inalenga kuimarisha pakubwa uhusiano kati ya mataifa hayo ya Afrika Mashariki.

Aidha Mudavadi ameeleza kwamba ziara hiyo pia inalenga kufanya tathmini ya hatua zilizopigwa katika makubaliano ya awali kati ya nchi hizo jirani.

Masuala ibuka katika nchi za ukanda na kimataifa pia yatajadiliwa wakati wa kikao cha wakuu hao kutoka Kenya na Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.