Pata taarifa kuu

Kenya: Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko imeongezeka hadi 188 tangu Machi

Takriban watu 188 wamefariki, kulingana na ripoti ya hivi punde ya mafuriko iliyotolewa siku ya Alhamisi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya. Tangu kuanza kwa msimu wa mvua mwezi Machi, Kenya imekumbwa na hali mbaya ya hewa. Barabara zimefungwa, madaraja na mabwawa yameporomoka... idadi ya vifo kutokana na mafuriko haya ni kubwa na inatarajiwa kuongezeka zaidi.

Un pompier kényan lors des inondations, le 1er mai 2024.
Afisa wa kikosi cha Zima moto ch Kenya wakati wa mafuriko, Mei 1, 2024. AFP - LUIS TATO
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani, watu 90 bado hawajapatikana. Zaidi ya nusu yao ni waathiriwa wa tukio la kuporomoka kwa hifadhi ya maji huko Mai Mahiu, takriban kilomita mia moja kaskazini mwa Nairobi, usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu.

Leo, ni Masai Mara, mbuga kubwa ya kitaifa kusini-magharibi mwa nchi, ambayo ilihamasisha waokoaji. Tangu Jumatano, karibu watalii mia moja wamenaswa ndani ya maji. Mafuriko ya kijito cha Mto Mara yalisomba kambi na nyumba kadhaa za kulala wageni. Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limetangaza kuwa tayari limewaondoa zaidi ya wasafiri 90.

Madhara yake ni dhahiri yatakuwa makubwa kwa hifadhi hii, wanaonya wataalamu katika sekta hiyo. Masai Mara ni hifadhi muhimu ya wanyamapori wa Kenya.

Katika maeneo mengine ya nchi, Wizara ya Mambo ya Ndani sasa inakadiria kuwa watu 165,000 wamelazimika kuyahama makazi yao. Siku ya Jumanne, viongozi waliwaomba watu wanaoishi katika maeneo yaliyo hatarini kuhama mara moja, vinginevyo watatumia nguvu.u

Usimamizi wa kukabiliana na janga wakosolewa

"Mamlaka za Kenya zilishindwa kujibu ipasavyo mafuriko," Human Rights Watch iliandika katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi. Shirika hili lisilo la kiserikali linashutumu mwitikio wa kuchelewa kutoka kwa mamlaka na mahitaji duni, hasa katika vitongoji maskini vya Nairobi.

Kituo cha haki za kijamii huko Mathare, kitongoji duni katika mji mkuu, kwa mfano, kinahesabu karibu familia 200 waathirika wa mafuriko ambao hawajapata msaada kutoka kwa mamlaka.

Human Rights Watch pia inashangazwa na kutokuwa tayari kwa mamlaka za umma. "Katika mpango wake wa kitaifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi 2023-2027, Kenya hata hivyo inabainisha mafuriko kama tishio," inabainisha HRW.

Kufikia Mei 2023, serikali ya Kenya imetangaza kuwa itatenga shilingi bilioni 10 (takriban dola milioni 80) kukabiliana na hali mbaya ya hewa inayotarajiwa mwaka ujao. "Hata hivyo, ilishindwa kuweka mpango wa kitaifa kwa wakati," Human Rights Watch inashangaa.

Na sio HRW pekee. Taasisi ya watafiti wa Kenya au hata kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, haelewi ni kwa nini hali ya "maafa ya asili" bado haijatangazwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.