Pata taarifa kuu

Tahadhari yaendelea kuhusu kimbunga Hidaya nchini Kenya na Tanzania

Maeneo ya ukanda wa Pwani nchini Kenya na Tanzania, yanashuhudia upepo mkali, huku mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa, zikitoa tahadhari ya uwekezekano wa kutokea kwa kimbunga Hidaya, kitakachoambatana na mvua kubwa.

Wakati kimbunga kilipotokea kwenye kisiwa cha  La Réunion
Wakati kimbunga kilipotokea kwenye kisiwa cha La Réunion AFP - RICHARD BOUHET
Matangazo ya kibiashara

Nchini Tanzania, usafiri wa boti na vivuko kati ya Dar es salaam na Zanzibar zimesitishwa hadi siku ya Jumatatu, baada ya kutolewa kwa tahadhari ya maeneo ya Pwani kukumbwa na kimbunga hidaya.

Wakaazi maeneo hayo waliozungumza na RFI Kiswahili wamesema kuanzia jana walianza kushuhudi upepo mkali, huku kisiwa cha Mafia kikiathrika.

"Upepo mkali umekuwepo toka jana usiku," Steven Mumbi, mwandishi wetu wa Dar es salaam amesema.

Wataalam wanaonya  kuwa kimbunga hicho kinatarajiwa kuwa kikubwa, katika siku zijazo.

Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini Kenya siku ya Jumamosi imesema athari za kimbunga hidaya zimeanza kushuhudiwa kutokana na upepo mkali unaoendelea kuvuma, hali inayotarajiwa kuendelea kwa siku mbili zijazo.

Wakaazi wa maeneo ya Pwani ya nchi hizo mbili na Kusini mwa Tanzania,  wametakiwa, kuendelea kuchukua tahadhari.

Tahadhari ya kimbunga hiki inakuja, wakati huu Kenya na Tanzania zikiendelea kushuhudia mvua kubwa iliyosababisha mafuriko, yaliyoleta maafa ya zaidi ya watu 400 na maelfu kulazimika kuyahama makaazi yao baada ya kusombwa na maji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.