Pata taarifa kuu

Kenya: Hamsini wauawa baada ya bwawa kupasuka kaskazini mwa Nairobi

Takriban watu 50 wamefariki dunia nchini Kenya baada ya bwawa kupasuka kaskazini mwa mji mkuu Nairobi, huku nchi hiyo ya Afrika Mashariki ikiendelea kukumbwa na mvua kubwa na kusababisha vifokadhaa na uharibifu mkubwa.Β 

Mtazamo wa angani wa nyumba zilizoharibika baada ya mafuriko makubwa kuharibu nyumba kadhaa wakati bwawa lilipopasuka, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika kijiji cha Kamuchiri, Mai Mahiu, Kaunti ya Nakuru, Kenya mnamo Aprili 29, 2024.
Mtazamo wa angani wa nyumba zilizoharibika baada ya mafuriko makubwa kuharibu nyumba kadhaa wakati bwawa lilipopasuka, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika kijiji cha Kamuchiri, Mai Mahiu, Kaunti ya Nakuru, Kenya mnamo Aprili 29, 2024. REUTERS - Edwin Waita
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, GaΓ«lle Laleix

Nchini Kenya, takriban watu hamsini wamefariki baada ya bwawa kupasuka. Haya yalitokea usiku wa Jumapili Aprili 28 kuamkia Jumatatu Aprili Β 29 huko MaΓ― Mahiu, kaunti ya Nakuru, takriban kilomita mia moja kaskazini mwa Nairobi. Mvua kubwa iliyonyesha usiku kucha ilisababisha bonde hilo kufurika na lambo kuharibiwa.

Katika eneo la Ngueiya, kijiji kilio chini ya mto kutoka kwa bwawa, ni mandhari ya ukiwa, kukiwa na maporomoko makubwa ya matope, na miti iliyong'olewa na mawe ambayo yameviringika kutoka mlimani. Kuna hata gari ndogo aina ya 4X4 iliyopaishwa kwenye matawi ya mti.

Chini ya kichungi, katika ua wa shule ya msingi ya Ngueiya, Joseph bado yuko katika mshtuko. Ilikuwa karibu saa 9 usiku ambapo mafuriko yalipiga nyumba yake: "Nilikuwa kitandani kwangu na nikasikia sauti ya nje. Nilitaka kutoka lakini mlango wangu ulizuiwa na maji. Maji yalijaa katika nyumba yangu, ghafla ikasombwa. kila kitu kikazamishwa majini. Kila kitu, hata kuta. Hakuna kilichobaki. "

Ann anatoka katika kijiji cha Jerusalemu. Familia yake ndiyo pekee iliyookoka. Mito hiyo ilipowachukua watoto wake, alifikiri kwamba hatawaona tena: β€œWalicsombwa na maji. Sote tulitenganishwa. Nilisikia watoto wangu wakipiga kelele kwa mbali. Baada ya kama dakika ishirini nilianza kuogelea. Nilimkuta binti yangu mmoja amelala juu ya mti, nikamuokoa. Niliogelea tena kumchukua binti yangu mwingine. "

Kwa wakati huu, hakua matumaini ya kuwapata waathirika. Waokoaji na majirani wanaendelea kutafuta miili ya watu waliotoweka. David Aderasu, kutoka shirika lisilo la kiserikali la Saint John Ambulance, alipata watu kadhaa waliofariki: β€œNilipata miili hapa, kuelekea Mai Mahiu, chini, kwa sababu ilibebwa na maji. Baadhi walikuwa wakielea, wengine walikuwa wamekwama kwenye matope. Kuna timu nyingine, chini kidogo, inaendelea kuchimba kuopoa miili ambayo bado imekwama. "

Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya, watu 49 bado hawajapatikana.

Hii si mara ya kwanza kwa kaunti ya Nakuru kushuhudia janga kama hilo: mnamo mwaka 2018, kuporomoka kwa bwawa la Solait kulisababisha karibu waathiriwa hamsini. Hali ilikuwa kama sawa kabisa: mvua kubwa ilisababisha mafuriko na kisha uharibifu.

Mapema siku ya Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Ndani alitangaza kuwa mabwawa yote nchini yatafanyiwa ukaguzi ndani ya saa 24. Kwa sababu hapa, mvua zinaendelea na vimbunga vikali vinatarajiwa. Ufungzi wa mwaka wa shule uliokuwa umepangwa siku ya Jumatatu Aprili 29 umeahirishwa kwa wiki moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.