Pata taarifa kuu

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan kwa Waislamu umeanza

Nairobi – Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan kwa Waislamu unaanza leo Jumatatu, Saudi Arabia na mataifa mengine ya Mashariki ya Kati yametangaza, huku hali ya vita vikali ikishamiri huko Gaza. Wakati mataifa mengine kama Oman yakitarajiwa kuanza hapo kesjho Jumanne.

Ramadhani ni moja ya nguzo tano za Uislamu.
Ramadhani ni moja ya nguzo tano za Uislamu. AP - Michael Probst
Matangazo ya kibiashara

Saudi Arabia, ambayo ni makazi ya maeneo matakatifu zaidi ya Uislamu, imesema kupitia shirika lake rasmi la habari la SPA Jumapili kwamba Mahakama ya Juu ilitangaza "Jumatatu, Machi 11, 2024, mwanzo wa mwezi uliobarikiwa wa Ramadan kwa mwaka huu".

Ramadhani ni moja ya nguzo tano za Uislamu.Baada ya kuonekana kwa mwezi mpevu, Umoja wa Falme za Kiarabu na Qatar pia zilitangaza kuanza kwa Ramadan Jumatatu kupitia vyombo vyao rasmi vya habari. Baraza la ushauri la Kiislamu la Misri Dar al-Ifta pia lilithibitisha kuwa Ramadhani inaanza Jumatatu, kama itakavyokuwa katika Mikoa ya Palestina ikijumuisha Gaza, na Algeria na Tunisia.

Oman pia itaadhimisha siku ya kwanza ya Ramadani Jumanne
Oman pia itaadhimisha siku ya kwanza ya Ramadani Jumanne AP - Mahmoud Illean

Majirani zao Morocco na Libya wao walisema Ramadhani itaanza Jumanne. Awali Iran ilikuwa imeweka mwanzo wa Ramadan kwa Jumanne baada ya ofisi yake ya uchunguzi wa mwezi ya "Estehlal" kusema kuwa haikuwezekana kuadhimisha "mwezi wa mwezi wa Ramadhani".

Huko Saudi Arabia, kuanza kwa mwezi mtukufu kumetiwa shaka baada ya baadhi ya vyombo vya uchunguzi vya ufalme huo kuripoti kwamba mwezi ulifichwa na "hali ya hewa ya mawingu na chembe za vumbi". Lakini uthibitisho wa mwisho wa muandamo huo ulikuja kupitia Chuo Kikuu cha Al Majmaah Astronomical Observatory huko Riyadh.

Alipotangaza Jumanne kama mwanzo wa Ramadan nchini Jordan, Mufti Mkuu wa ufalme huo Ahmed Hasnat alimwomba Mwenyezi Mungu "kuondoa uchungu wa watu wetu wanaokandamizwa huko Gaza" na "kuondoa mateso na uchokozi kutoka kwao".

Sehemu kubwa ya waisilamu duniani wanaanza mfungo wao hivi leo Jumatatu.
Sehemu kubwa ya waisilamu duniani wanaanza mfungo wao hivi leo Jumatatu. REUTERS - Hasnoor Hussain

Oman pia itaadhimisha siku ya kwanza ya Ramadani Jumanne. Wakati wa Ramadan, Waislamu waangalifu hujizuia kula na kunywa kuanzia alfajiri hadi jioni, na kwa desturi hukusanyika pamoja na familia na marafiki ili kufuturu jioni.

Pia ni wakati wa sala, wakati waumini hukusanyika kwa wingi misikitini, haswa nyakati za usiku. Vita kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza vimeleta kivuli kirefu kuhusu sherehe katika eneo hilo, huku matumaini yakiwa yamefifia kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano yanaweza kufikiwa kabla ya Ramadhani kuanza.

Waisilamu wanafunga kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Waisilamu wanafunga kwa kipindi cha mwezi mmoja. REUTERS - Amr Abdallah Dalsh

Katika soko la Rafah, kusini mwa mji wa Gaza ambapo karibu watu milioni 1.5 wametafuta hifadhi, Wapalestina Jumapili waliomboleza uhaba wa chakula na kutokuwa na uhakika wa wakati wa vita juu ya mwezi mtukufu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.